Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 19, 2014

Yanga yaingia kambini kuiwinda Ruvu Shooting


Ruvu Shooting
Yanga
KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo imeingia kambini mjini Bagamoyo kwa ajili ya pambano lao lijalo dhidi ya Ruvu Shooting litakalochezwa siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji 28 bila Hussen Javu anayesumbuliwa na Malaria ndiyo walioingia kambini kwa ajili ya mechi hiyo ambayo Ruvu wametamba kuinyoa vijana wa Jangwani kama anavyotamba Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire.
Kambi hiyo pia inaelezwa itakuwa ikitumiwa na Yanga kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika, dhidi ya Al Ahly ya Misri mechi itakayochezwa Machi Mosi kwenye uwanja wa Taifa.
Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alinukuliwa hivi punde na Radio One Stereo, amekiri timu yake kuingia kambini kwa ajili ya mechi ya Ruvu na ile ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika.
Kizuguto alisema wachezaji wote wana ari ya ushindi, huku msemaji mwenzake, Masau Bwire amesema kuwa Yanga lazima waanze kuchagua mapema aina ya mnyoo watakaonyolewa Jumamosi kama ni Kiduku au kipara kwani hawatapona Jumamosi wakitambia kocha wao Tom Oloba na wachezaji wake mahiri.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza Yanga ikiwa wenyeji, Ruvu walikaa kwa kulala bao 1-0, kitu ambacho Bwire ametamba ni lazima walipize kisasi kwa vijana hao wa Johannes van der Pluijm. Ngoja tuone inakuwaje

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...