Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 2, 2014

TAIFA STARS YASONGA MBELE KWA JUMLA YA MABAO 3-2 DHIDI YA ZIMBABWE, SASA KUKUTANA NA MSUMBIJI


 Pichani (kulia) ni Winga wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Simon Msuva, akimtoka beki wa Zimbabwe, wakati wa mchezo huo uliopigwa jana, jijini Harare.
**************************************
TIMU ya Taifa Taifa Stars, jana imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2015) baada ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zimbabwe.

Kwa matokeo hayo sasa Stars imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 kutokana na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutinga katika hatua ya pili sasa Stars inatarajia kukutana na Msumbiji wiki mbili zijazo ambapo ikifanikiwa kupita hatua hiyo itaingia katika hatua ya makundi.

Mabao yaliyoiwezesha Stars kusonga mbele katika mchezo wa jana yalifungwa na Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 26, na Thomas Ulimwengu katika dakika ya 46, huku mabao ya wenyeji yakifungwa na Danny Phiri katika dakika ya 13 na Willad Katsande katika dakika ya 55.

Baada ya kumalizika dakika 90 za mchezo huo, Mwamuzi aliongeza dakika saba, lakini bado hali ilionekana kuzidi kuwa ngumu kwa wenyeji waliokuwa wakitafuta bao la kuongoza ili angalau kujaribu kujitetea kwa matuta.

Katika mchezo ujao unaoikabiri Stars, iwapo Msumbiji wakitolewa Stars itatinga moja kwa moja katika kundi F lenye timu za Zambia, Cape Verde na Nigeria.
 Wachezaji wa Taifa Stars wakijipa morali ya ushindi kabla ya kuanza kwa mtanange huo dhidi ya Zimbabwe jana. 
 Sehemu ya mashabiki wa Taifa Stars walioambatana na timu na baadhi ya Watanzania waishio Harare, wakishangilia kuisapoti Taifa Stars jana.
 Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka beki wa Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...