Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 1, 2013

Shabiby yaidhamini habari Group

MBUNGE wa jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby ambaye ni mmiliki wa kampuni
ya mabasi, Shabiby Line Bus Services, ametoa udhamini kwa kikundi cha
Waandishi wa Habari Wajasiriamali (Habari Group), watakaotembelea
bunge mjini Dodoma wiki hii.

Habari Group wamepata mwaliko wa kutembelea Bunge, kutoka kwa Naibu

Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki.

Angellah pia ni mlezi wa kikundi hicho, ambapo pamoja na mambo

mengine, Habari Group watakuwa na mkutano na mlezi huyo  na wadau
mbalimbali wakiwemo wabunge kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya
kikundi.

Akizungumzia udhamini huo, Shabiby alisema ameguswa na malengo ya

kikundi hicho, na kuamua kukisaidia kama mchango wake kwa maendeleo ya
taifa.

Alisema, kwa kuwa kampuni yake ni ya kizalendo, kusaidia makundi kama

Habari Group ni moja ya majukumu ya Shabiby Line.

Mwenyekiti wa Habari Group, Mwanamkasi Jumbe, alishukuru kwa udhamini

huo, ambao unahusisha usafiri na kwamba inawapa moyo kuona viongozi na
wafanyabiashara mbalimbali kuunga mkono juhudi za wasichana, hasa
wenye malengo ya kujikomboa.

Alisema waandishi wa habari wengi wamekuwa hawana malengo, na mwisho

wa siku kuishia pabaya, lakini wameamua kujikusanya na kuweka akiba
zao kwa manufaa ya baadaye.

Alimsifu Angellah, ambaye amekuwa akijitolea kwa kiasi kikubwa

kuhakikisha kikundi hicho kinasonga mbele, na kuomba wadau mbalimbali
kujitokea na kusaidia makundi kama hayo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...