Miss
Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha wakati
akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na
watatu Esther Mussa, baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo
lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza
Jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa
Sufianimafoto.blogspot,com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi
zawadi Maria John, baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumska
Sufianimafoto Miss Talent, lililofanyika ndano ya shindano hilo la Miss
Sinza katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.
Sufianimafoto Miss Talent, Maria John, akiwa na furaha baada ya kuvishwa taji hilo na kukabidhiwa zawadi yake.
Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) akiwa na
baadhi ya wanakamati wakishuhudia shindano hilo.
Mshiriki, Nancy, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
![]() |
Mshiriki,Naima mohamed, akipita jukwaani na vazi la ufukweni. |
Mshiriki, Maria John, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Msanii
wa Vichekesho, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo Kweli,
akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo na kuwapagawisha vilivyo,
mashabiki wa fani ya urembo waliokuwapo ukumbini hapo.
No comments:
Post a Comment