Bondia
David Haye (kushoto) akimpeleka chini, Dereck Chisora, baada ya
kumaliza pambano hilo kwa KO katika raundi ya tano katika pambano lao
lililopigwa jana usiku. ***************************************** |
BINGWA
wa zamani wa dunia uzito wa juu, David Haye, amemaliza kazi kwa
kumfunga mdomo mpinzani wake Chisora, baada ya kumchapa katika raundi ya
tano ya mchezo huo uliokuwa na msisimko mkubwa kutokana na wapinzani
hao kutambiana na kutishiana kuchapana wakati wakipima utizo juzi.
Pambano
hilo lililosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa masumbwi na hasa
kutokana na kuchelwa kutokana na utata wa vibali wa mabondia hao
waliokuwa wamefungiwa kupigana na mamlaka za ngumi.
Katika
pambano hilo, Haye, alionekana kutawala pambano hilo kwa kuanza kwa
kasi ya ajabu tangu mwanzo wa raundi ya kwanza huku akionekana kujiamini
zaidi na kumfanya Chisora kushindwa kabisa kujibu mashambulizi hadi
ilipofika raundi ya tatu alipofanikiwa kurusha ngumi ya kwanza na ya
maana usoni mwa Haye.
Chisora
ambaye kabla ya pambano hilo, alikuwa akijigamba zaidi kwa tambo nyingi
akidai kumchapa Haye na kwamba ataingia katika pambano hilo kama
'kichaa' na kuweka ahadi kuwa angemdondosha Haye katika raundi ya saba.
usemi
wake huo ulikuwa ni kinyume kwani yeye ndiye aliyeweza kupelekwa chini
mara mbili katika raundi ya tano na mchezo huo ukamalizika katika
raundi hiyo ya tano baada ya kuhesabiwa na kusimama lakini akionekana
kushindwa kuendelea na pambano hilo.
Muda
mfupi baada ya kuruhusiwa kuendelea na pambano, Haye hakutaka kumpa
muda wa kurejea katika hali yake ya kawaida, akamfuata haraka na
kuendelea kushambulia. Ngumi tano mfululizo zilizoingia kwenye taya na
usoni zilimpeleka chini Chisora ambaye wakati akijaribu kuinuka, refa
alimaliza pambano.
Kwa
ushindi huo, Haye aliongeza rekodi ya mapambano yake kuwa ameshinda 26
(24 kwa KO) na amepigwa mawili hajatoka sare, wakati Chisora sasa
amepigwa mara 4, ameshinda 15 (9 kwa KO) na hajatoka sare.
Chisora akipokea konde zito la taya la kushoto kutoka kwa Haye.
No comments:
Post a Comment