Mwandishi
Mwandamizi wa Habari za Michezo, Chris Mwambonda amefariki usiku wa
kuamkia leo jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa
Marehemu Mwambonda, Mawazo Lusonzo, mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika hospitali ya Mwananyamala na mipango ya maziko inafanyika
nyumbani kwa mama yake mzazi Goba na mipango ya mazishi inafanyika huko
huko, taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Pichani ni moja katika ya
matukio aliyoshiriki enzi za uhai wake ambapo hapa anaonekana
akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo yaliyowashirikisha wahariri
wa michezo na Mkurugenzi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leonard
Thadeo baada ya semina ya wahariri wa michezo iliyofanyika Juni 10 2010.
No comments:
Post a Comment