Washindi wa Tuzo tatus za Zuku
zilitangazwa wakati wa kufungwa rasmi wa tamasha la ZIFF. Tuzo za Zuku
ni jamii mpya za tuzo ambazo zimefanikishwa kwa mara ya kwanza katika
Tamasha la ZIFF. Tuzo hizo zili wazawadia filamu zenye ubunif wa
kuelezea hadithi za kiafrika, zilizotengenezwa Afrika, na watengenezaji
na wasanii kutoka bara la afrika.
Akizungumza
wakati wa kutoa tuzo, Wangeci Murage Zuku alisema, "Tunafurahia sana
kuanzisha tuzo mpya katika tamasha la ZIFF na lengo letu ni kukuza tuzo
hizi hadi ziwe mojawapo wa tuzo za kifahari hapa Afrika”.
Mwaka huu, tuzo la Zuku Best African Film Award lilipewa filamu ya ‘Inside Story’ kutoka Rwanda iliyotayarishwa na Rolie Nikiwe. Tuzo la Zuku Best Actor Tuzo lilishindwa na mwigizaji Kevin Ndege Mambo ambaye alifanya kazi kama katika filamu ya ‘Inside Story’. Tuzo la Zuku Best Actress lilishindwa na waigizaji wanawake watatu yaani Thuli Khulamelo, Nomfundo Dunazana na Reona Ngiba ambaye waliigiza katika filamu ya ‘Uhlanga the mark’
Tuzo za Ousmene Sembene Award and Verona Award na Tuzo la ZIFF Golden Dhow Award zilishindwa na mfilmau ya ‘Uhlanga the mark’. Tuzo la ‘ZIFF Best Short Film’ lilishindwa na Filamu ‘Mocassin’ iliyotayarishwa na Denis M. Kimathi. Tuzo la ZIFF Best Documentary Award, lilishindwa na filamu ya “Mama Africa” iliyotayarishwa na Mika Kaurismaki. Tuzo la ZIFF Best Animation Award lilipewa “Ostora” iliyotayarishwa na Hani Kichi
Kwa upande wa filamu za Tanzania, ‘Zamora’ iliyotayarishwa na Shams Bhanji iliweza kutwa tuzo mbili za filamu bora afrika mashariki na filamu. Filamu ya “Chungu” iliyotayarishwa na Kiela Billa iliwea kutwaa tuzo ya filmau bora ya ZIFF.
Zuku
ambayo ni kampuni ya TV ya kulipia ambayo inaendelea kukua kwa kasi
inapatikana Tanzania, Uganda na Kenya, ina nia ya kudhamini ZiFF kwa
kipindi cha miaka 10 kwa thamani ya jumla ya dola milioni moja. Udhamini
huo unatarajiwa kutoa utulivu na msaada ambayo kwa upande utachangia
kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya filamu, si tu nchini
Tanzania lakini maeneo mengine ya Afrika.
Kingamuzi
cha Zuku kinatoa wigo mpana wa uchaguzi wa burudani ka vile habari za
michezo, sinema, makala na muziki. Hizi ni pamoja na chaneli tatu za
BBC World News, MTV Base, Setanta Sports, Fox Entertainment na E!. Zuku
pia inatoa chanelli zingine kama Zuku AFrika, Zuku Life, Zuku Sports na
Zuku Movies. Huduma hii patikana kupitia satellite mahali popote
Tanzania
No comments:
Post a Comment