YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS -TPBO
NDG WAANDISHI NA WADAU WA MICHEZO WOTE KWA UJUMLA WETU,
AWALI YA YOTE NAPENDA KUTUMIA FURSA HII KUMPONGEZA BONDIA BINGWA WA
DUNIA WA WBF,FRANCIS CHEKA KWA KUKUBALIANA NA WAZO LANGU LA KUMUOMBA
AJIUNGE NA KUWA MIONGONI MWA WATANZANIA WATAKOJITOKEZA TAREHE 08-12-2013
JIJINNI DAR-ES0SALAAM KUUNGANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA
TANZANIA MH, JAKAYA MRISHO KIKWETE KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON ZENYE
KUADHIMISHA UHURU WA TANGANYIKA.
KWA KWELI NILIKUWA NA MATEGEMEO MAKUBWA SANA KWAMBA FRANCIS CHEKA
ANGENIKUBALIA WAZO LANGU HILO ,AKIWA KAMA NI MTANZANIA ANAYEIPENDA KWA
DHATI NCHI YAKE KWANI AMESHAIPATIA SIFA KUBWA TANZANIA KWA KUTWAA TAJI
LA UBINGWA WA NGUMI WA DUNIA DHIDI YA MMAREKANI PHILL WILLIAM HAPO
TAREHE 30-08-2013 .
NA NILISHAWISHIKA KUMSHAURI CHEKA AINGIE KWENYE MBIO HIZI BAADA YA
KUVUTIWA NA TAARIFA ZA WAANDAAJI KWAMBA KATIKA MBIO HIZO YUMO BINGWA WA
DUNIA WA MBIO HIZO KUTOKA KENYA, NIKAONA IKO HAJA KWA MABINGWA WA
TASNIA ZISIZOFANANA WAKANOGESHA MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON HAPO
08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.
NINAONA WAZI KWAMBA SASA IPO HAJA HATA KWA MAKAMPUNI MBALIMBALI
YAKAMTUMIA FRNCIS CHEKA KATIKA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI ZA KIJAMII NA
HATA KUWATANGAZIA BIASHARA ZAO.
KWA KWELI HIZI NI MBIO AMBAZO ZINAPASWA KUUMGWA MKONO NA KILA MTANZANIA
NA SIYO WANARIADHA PEKEE ,KWANI HAYATI BABA WA TAIFA HILI MWL JULIUS
KAMBARAGE NYERERE ALIUPIGANIA UHURU WA NCHI HII KWA MASLAHI YA
WATANZANIA WOTE, BILA KUJALI ITKADI ZA KIDINI, ZA KIMICHEZO ,NA HATA
UKABILA.
NI JAMBO LA KUTIA MOYO KWAMBA WAMEJITOKEZA WATANZANIA WENYE NIA NJEMA
KABISA YA KUUENZI UHURU WA TANGANYIKA KWA NJIA YA MICHEZO [KAMA HAWA
WAANDAAJI WA UHURU MARATHON].
NI LAZIMA TUWAUNGE MKONO WAANDAAJI HAWA KWA HALI NA MALI ILI TUUENZI VYEMA UHURU WETU.
NINATUMIA FURSA HII KUWAOMBA MABONDIA WENGINE NA WADAU WA MCHEZO WA
NGUMI WAJIUNGE KWENYE MBIO HIZI KWA LENGO MOJA TU NALO NI KUUENZI UHURU
WA NCHI YETU ,KWANI BILA KUWA NA UHURU KTK NCHI YOYOTE , WAZALENDO WA
NCHI ILE HUWA HAWANA TOFAUTI NA WATUMWA,KWANI WANAKUWA HAWANA MAAMUZI
YAO BINAFSI ,KWA KUWA KILA JAMBO HUAMULIWA NA WATAWALA WAO BILA KUJALI
JAMBO NI ZURI AU BAYA.
KWA KUWA WAANDAAJI WAMETUTANGAZIA KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI
KWAMBA KUNA MATAIFA ZAIDI YA 21 YAMETHIBITISHA KUSHIRIKI KATIKA UHURU
MARATHON ,PIA MHESHIMIWA RAIS,NA WABUNGE , WAMETHIBITISHA USHIRIKI
WAO,SIONI KWA NINI WATANZANIA WA KAWAIDA TUSISHIRIKI KATIKA TUKIO HILI
LA KIHISTORIA LA UHURU MARATHON.
PIA NINAYAOMBA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAZIDHAMINI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON KILA MWAKA ,NA ISIWE MWAKA HUU PEKEE.
NINA IMANI KUBWA SANA KWAMBA WATANZANIA WENGI TUTASHIRIKI MBIO HIZI ZA
UHURU MARATHON SIKU HIYO YA TAREHE 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE ,NA UDUMISHE UHURU NA AMANI NCHINI KWETU TANZANIA.
IMELETTWA KWENU NAMI;-
YASSIN ABDALLAH -USTAADH
RAIS; TPBO-LTD
+255 713-644974 752 335584