Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 7, 2013

MABONDIA MBELWA VS KAONEKA KUPIMA UZITO JUMAMOSI AMANA CCM


MABONDIA Said Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na Shabani Kaoneka 'BSS'  watapima uzito siku ya jumamosi ya tarehe 9 novemba  utakaofanyika  Amana CCM Ilala  kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya tarehe 10 novemba  mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Zulu Paradais Pugu Kilumba, akizungumzia mpambano huo mratibu ambaye pia ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamla 'Super D' amesema kila kitu kimesha kamilika kilichobaki ni kupima uzito siku ya jumamosi ambapo mabondia hawo wanatakiwa wawe na KG 76 kila mmoja kwa ajili ya mpambano huo wenye upinzani wa ali ya juu kutokana na kila mmoja kujigamba kuwa atamtwanga mwenzie raundi za awali mabondia hawo waliokuwa wakitafutana kwa mda mrefu sasa tunahesabu masaa macheche kwa ajili ya mpambano wao wa raundi 8 mbali na mbambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo bondia Hamza Mchanjo atamenyana na Tony King wakati Chirambo Hemed atafaana na Sharifu Mzezele nae Twalibu Mchanjo atapambana na Mohamed Kashinde uku bondia Adamu Ngange atapambana na Shabani Mtengela 'Zunga Boy'   mbali na kuwepo kwa mapambano hayo siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa DVD mpya za bondia Said Mbelwa ambapo alipocheza nje ya nchi zikiwemo ujerumani, afriganstan pamoja na DVD za ngumi kali mbazo zitakuwa zikiuzwa kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini pia kutakuwa na vifaa mbalimbali vikiuzwa kwa bei nafuu kwa wadau wa mchezo wa ngumi kama vile, clip bandeji,gum shit,bukta, glove na vifaa mbalimbali vya masumbwi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...