
Mabondia
Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini
Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21
Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa
katika pambano la kirafiki lisilo la ubingwa..

Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano
hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa, pia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi.
Mabondia
wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby
Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza
na Shah Kassim, kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis
mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae mbena Rajabu.
Wengine ni Issa Omar atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera.
Mabondia
wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia
kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya
juu.
kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment