Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, November 19, 2013

BAADA YA KUPATA UBUNGE BONDIA Vitali Klitschko ‘Dr. Ironfist’ SASA ATAMANI URAIS


Klitschko: Nina kiu ya Ikulu
MIAKA ya hivi karibuni wanamichezo na wasanii nchini ikiwamo na wale wa nje ya nchi wamezinduka wakijitosa kwenye masuala ya kisiasi kama udiwani, ubunge, ugavana na hata ngazi ya juu ya urais. 
Leo katika maisha ya wenzetu tutaangazia maisha ya ya mbabe Vitali Klitschko ‘Dr. Ironfist’ bingwa wa uzito wa juu wa WBC, aliyetangaza azma yake kuwania urais wa nchini Ukraine katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Katika taarifa yake na wanahabari anasema: “Nahitaji kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, hakuna anayeweza kunizuia kugombea,”
Klitschko (42), anasema: “Ingawa nimekuwa nikiishi nchini Ujerumani, kwangu naona hilo si tatizo la kunizuia kuwania urais wa nchi hiyo kwa mujibu wa Katiba kwani ninabaki kuwa raia wa Ukraine.”
Mbabe huyo yuko katika rekodi ya wababe wa uzito wa juu wanaotambuliwa na WBO kwa kufanikiwa kutwaa mikanda mitatu ya ubingwa wa dunia, wengine wakiwa Muhammad Ali, Evander Holyfield na Lennox Lewis.
Usichokijua
Mbabe huyo mwaka 2006 aliwahi kuwania umeya wa Kiev lakini alijikuta akibwagwa na mwaka 2008 alifanikiwa kutwaa umeya wa halmashauri ya Kiev.
Mwaka jana alifanikiwa kuwa mbunge wa Bunge la Ukraine kupitia chama cha UDAR.
Mwaka 2005 wakati akimchapa Hashim Rahman na kutwaa ubingwa wa WBC alitangaza kustaafu mchezo huo,  lakini Januari 24, 2007 alitangaza kurejea upya.
Ndiye mbabe ambaye anatarajiwa kubadili mawazo ya Lenox Lewis ya kustaafu, kutokana na hivi karibuni Lewis kutangaza kwamba iwapo atatokea mdhamini mwenye dola milioni 100 za kumlipa ataingia kucheza na Vitali.  
Mahusiano
Mbabe huyo na mkewe Natalia Egorova aliyekuwa mwanariadha na mwanamitindo wamebarikiwa kuwa na watoto watatu ambao ni Yegor (Daniel), Elizabeth (Victoria) na Max.
Utajiri
Mbabe Vitali Klitschko anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 65; fedha ambazo nyingi zake amezipata kupitia masumbwi, siasa na nyingine katika matangazo ya kampuni ya Ambergo na kampuni ya Shiatzy Chen na kuna wakati alikuwa akivaa nguo ya chini yenye nembo ya D-Star 200.
Vyakula
Mbabe huyo anatumia kiasi cha dola 20 kwa siku kwa ajili ya chakula anachokuwa anakula. Ikiwa ni kaa, mbogamboga na vingine vyenye asili ya Ukraine.
Usafiri
Ana magari kama Cadillac Escalade alilonunua kwa dola 75,000 na pia anayo nyingine inayokwenda kwa jina la 4Porsche Carrera GT aliyonunua kwa dola 440,000.
Nyingine ni Lexus LS 460 Sedan alilonunua kwa dola 60,000. Mercedes-Benz S65 lilomgharimu dola 210,000.
Jengo
BONDIA huyo anamiliki jengo lake katika maeneo ya Berlin, Ujerumani, likiwa limemgharimu kiasi cha dola milioni 11.
Jengo lake jingine liko Ukraine likiwa katika maeneo ya Kiev likiwa limemgharimu kiasi cha dola milioni 5.
Mawasiliano
Kwa masuala ya mawasiliano ya mwanamasumbwi huyo unatakiwa kutembelea website yake ambayo ni www.klitschko.com/vitali.
Wasifu
JINA: Vitali Volodymyrovych Klychko
UZITO: Futi 6 inchi 7
TAIFA: Ukraine
UMRI: 42
Makala hii imeandaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mitandao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...