Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 11, 2013

Muumin kuvunja ukimya, kuibukia wapi?


 http://4.bp.blogspot.com/-r_aUt9ALoMY/UMsDDTV1IgI/AAAAAAAAAwM/-Xhbog3qmMU/s1600/Muumini+huyu.jpg
MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa dansi nchini, Mwinjuma Muumin 'Kocha wa Dunia', amesema ataweka bayana  mipango yake kimuziki  wiki hii baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu tangu alipoachana na bendi ya Victoria Sound 'Wana Gusa Gusa'.
Muumin, alisema tangu alipoachana na bendi hiyo aliyokuwa akiiongoza baada ya kutokea ugomvi baina yake na mwanamuziki mwenzake, Wazir Sonyo, aliamua kupumzika muziki na kutuliza akili yake kwa kutembea mikoani na atarajea wiki hii toka Kahama kuvunja ukimya.
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya simu toka Kahama, Shinyanga, Muumin alisema atakuja kuweka bayana kitu gani kitafuata baada ya ukimya wake huo kwa sababu amekuwa wakiulizwa sana na mashabiki wake kuhusu shughuli zake za muziki.
"Mashabiki wamekuwa wakihoji ukimya wangu na wengine kudhani labda nipo huku mkoani nikifanya muziki, hapana nimekuja kupumzika tu na nijirudi Dar nitaweka bayana mustakabali mzima kuhusu wapi nitakapoibukia," alisema Muumin.
Mtunzi na muimbaji huyo nyota aliyewahi kutamba na bendi mbalimbali kama The Bantu Group, Africans Revolution 'Wana Tamutamu', Mchinga Sound, Double M Sound na nyingine alisema muziki ni fani yake na hawezi kuachana nayo ila alikuwa mapumzikoni kujipanga.
Kabla ya kutibuana na Victoria Sound, Muumin anayefahamika pia kwa jina la Mzee wa Chelsea alikuwa akimiliki bendi yake iitwayo Bwagamoyo International 'Wana Gusa Unase'.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...