Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 13, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAKAMU DKT. BILAL WAIFARIJI FAMILIA YA MUSSA SAMIZI Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu, Mussa Samizi, Bi. Misingo Samizi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam, leo mchana. Marehemu Samizi alikuwa ni Mtumishi Mstaafu wa Umma,aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi CCM na Serikali. Marehemu anazikwa leo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya marehemu, Mussa Samizi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tegete jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kutoa pole.
Rais, Jakaya Kikwete, akimfariji mke wa marehemu, Mussa Samizi, Bi. Misingo Samizi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam, leo mchana. Marehemu Samizi alikuwa ni Mtumishi Mstaafu wa Umma,aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi CCM na Serikali. Marehemu anazikwa leo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya marehemu, Mussa Samizi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tegete jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kutoa pole.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...