Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 11, 2013

HATIMAE JACKLINE WOLPER AFUNGUKA BAADA YA KUBADILI DINI KWA MARA YA PILIHatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.

“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”

Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...