Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 11, 2013

NBC YAWAZAWADIA WASHINDI WA PROOSHENI YA WEKA UPEWE


 Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto), akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wengine kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Mkuu wa Idara ya Huduma za Rejareja za Kibenki , Mussa Jallow, Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza,  Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Abdallah Hemedi. Wateja wanne walishinda pikipiki na wawili jenereta.
 Mkuu wa Idara ya Huduma za Rejareja za Kibenki wa Benki ya Taifa ya Biashara ( NBC) , Mussa Jallow (katikati) akizungumza wakati wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo,  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza,  Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Abdallah Hemedi. Wateja wanne walijishindia pikipiki na wawili jenereta.
 Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC,  Dorothea Mabonye (katikati) akibonyeza kompyuta  ili kumpata mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyojijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow  na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Abdallah Hemedi. Wateja wanne walijishindia pikipiki na wawili jenereta.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC na waandishi wa habari wakifuatilia hafla ya droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. 
 Meneja Mahusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara ( NBC), Eddie Mhina (kushoto) akizungumza wakati wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake  ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo,  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Mkuu wa Idara ya Huduma za Rejareja za Kibenki, Mussa Jallow na Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza,  Dorothea Mabonye.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...