Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 29, 2013

JOSE CHAMELEONE ASAINI KUPIGA SHOW MOJA DEC 24 MKESHA WA CHRISTMAS JIJINI MWANZA


Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika mnamo tarehe 24/12/2013 mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza.

Picha zaidi za Mwanamuziki mkali Afrika akisaini mkataba baina yake na viongozi waandaaji wa Show hiyo. Makubaliano haya ya kuweka mkataba yamefanyika jumatatu ya wiki hii tarehe 25/11/2013 jijini Kampalanchini Uganda.
Mwanamuziki Dr. Jose Chameleone (katikati) akiwa na Mapromota wa show itakayofanyika jijini Mwanza Dennis Mshema (Kushoto) na Mr. Ben Mwangi (kulia) mara baada ya utiaji wa saini wa kupiga show moja kali tena takatifu itakayofanyika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas katika ufukwe wa Charcoal Ribs jijini Mwanza.
 Kwa mujibu wa moja wa Mapromota hao Mr. Ben amesema kuwa ile kiu ya mashabiki wa muziki wa ukweli toka kwa Mwanamuziki Jose Chameleone sasa inakwenda kupata dawa yake, kwani maandalizi mazuri yameanza kufanyika kuhakikisha kila kilichobora kina tukia kwenye jukwaa la burudani siku hiyo ya mkesha wa Christmas.

"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Alisema Ben.

 Ameongeza kuwa bado milango iko wazi kwa makampuni mbalimbali na sekta binafsi kushiriki katika suala zima la udhamini. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0752813212.

Mbali na kuwa na masongi makali kama Bei kali, Kamila na kadhalika ambayo hadi sasa utamu wake uko pale pale Jose Chameleone kwa sasa anatikisa ulimwengu wa burudani ya muziki na ngoma zake kali kama Badilisha, Sumula, Valu valu, Tubonge na nyingine kibao...

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...