Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, November 26, 2013

YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH AMPONGEZA CHEKA KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON RAIS -TPBO


                             YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                                                          RAIS -TPBO  
                  NDG WAANDISHI NA WADAU WA MICHEZO WOTE KWA UJUMLA WETU,

AWALI YA YOTE NAPENDA KUTUMIA FURSA HII KUMPONGEZA BONDIA BINGWA WA DUNIA WA WBF,FRANCIS CHEKA KWA KUKUBALIANA NA WAZO LANGU LA KUMUOMBA AJIUNGE NA KUWA MIONGONI MWA WATANZANIA WATAKOJITOKEZA TAREHE 08-12-2013 JIJINNI DAR-ES0SALAAM KUUNGANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA MH, JAKAYA MRISHO KIKWETE KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON ZENYE KUADHIMISHA UHURU WA TANGANYIKA.

KWA KWELI NILIKUWA NA MATEGEMEO MAKUBWA SANA KWAMBA FRANCIS CHEKA ANGENIKUBALIA WAZO LANGU HILO ,AKIWA KAMA NI MTANZANIA ANAYEIPENDA KWA DHATI NCHI YAKE KWANI AMESHAIPATIA SIFA KUBWA TANZANIA KWA KUTWAA TAJI LA UBINGWA WA NGUMI WA DUNIA  DHIDI YA MMAREKANI PHILL WILLIAM HAPO TAREHE 30-08-2013 .

NA NILISHAWISHIKA KUMSHAURI CHEKA AINGIE KWENYE MBIO HIZI BAADA YA KUVUTIWA NA TAARIFA ZA WAANDAAJI KWAMBA KATIKA MBIO HIZO YUMO BINGWA WA DUNIA WA MBIO HIZO KUTOKA KENYA, NIKAONA IKO HAJA KWA  MABINGWA WA TASNIA ZISIZOFANANA  WAKANOGESHA MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON HAPO 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.

NINAONA WAZI KWAMBA SASA IPO HAJA HATA  KWA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAKAMTUMIA FRNCIS CHEKA KATIKA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI ZA KIJAMII NA HATA KUWATANGAZIA BIASHARA ZAO.

KWA KWELI HIZI NI MBIO AMBAZO ZINAPASWA KUUMGWA MKONO NA KILA MTANZANIA NA SIYO WANARIADHA PEKEE ,KWANI HAYATI BABA WA TAIFA HILI MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIUPIGANIA UHURU WA NCHI HII KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE, BILA KUJALI ITKADI ZA KIDINI, ZA KIMICHEZO ,NA HATA UKABILA.

NI JAMBO LA KUTIA MOYO KWAMBA WAMEJITOKEZA WATANZANIA WENYE NIA NJEMA KABISA YA KUUENZI UHURU WA TANGANYIKA KWA NJIA YA MICHEZO [KAMA HAWA WAANDAAJI WA UHURU MARATHON].

NI LAZIMA TUWAUNGE MKONO WAANDAAJI HAWA KWA HALI NA MALI ILI TUUENZI VYEMA UHURU WETU.

NINATUMIA FURSA HII KUWAOMBA MABONDIA WENGINE NA WADAU WA MCHEZO WA NGUMI  WAJIUNGE KWENYE MBIO HIZI KWA LENGO MOJA TU NALO NI KUUENZI UHURU WA NCHI YETU ,KWANI BILA KUWA NA UHURU KTK NCHI YOYOTE , WAZALENDO WA NCHI ILE HUWA HAWANA TOFAUTI NA WATUMWA,KWANI WANAKUWA HAWANA MAAMUZI YAO BINAFSI ,KWA KUWA KILA JAMBO HUAMULIWA  NA WATAWALA WAO BILA KUJALI JAMBO NI ZURI AU BAYA.

KWA KUWA WAANDAAJI WAMETUTANGAZIA KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KWAMBA KUNA MATAIFA ZAIDI YA 21 YAMETHIBITISHA KUSHIRIKI KATIKA UHURU MARATHON ,PIA MHESHIMIWA RAIS,NA WABUNGE , WAMETHIBITISHA USHIRIKI WAO,SIONI KWA NINI WATANZANIA WA KAWAIDA TUSISHIRIKI KATIKA TUKIO HILI LA KIHISTORIA LA UHURU MARATHON.

PIA NINAYAOMBA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAZIDHAMINI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON KILA MWAKA ,NA ISIWE MWAKA HUU PEKEE.

NINA IMANI KUBWA SANA KWAMBA WATANZANIA WENGI TUTASHIRIKI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON SIKU HIYO YA TAREHE 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.


              MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE ,NA UDUMISHE UHURU NA AMANI NCHINI KWETU TANZANIA.


                                        IMELETTWA KWENU NAMI;-
                                       YASSIN ABDALLAH -USTAADH
                                       RAIS; TPBO-LTD
                                     +255 713-644974 752 335584

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...