Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 21, 2013

MAPACHA WATATU KUIACHIA YARABI NAFSI KESHO KWENYE BIRTHDAY YA MIAKA 4
BENDI ya Mapacha Watatu inayoongozwa na wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose  Mara’ kesho katika ukumbi wa  letasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar inatarajia kuzindua albam yake ya pili waliyoipa jina la Yarabi Nafsi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bendi hiyo Khamis Dakota alisema kuwa baada ya miaka mine yenye changamoto nyingi wameamua kusherehekea pamoja na wanamuziki wakongwe kutoka bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
Bendi ya Mapacha Watatu ina albamu mbili ambazo ni  Shika Ushikacho na Yarabi nafsi.
Dakota akizitaja nyimbo zilizomo katika albamu yao ya pili Yarabi Nafsi  ni pamoja na Yarabi Nafsi uliobeba jina la albamu, Ujasiriamali, Naonewa, Chanzo Wanaume, Sumu Ya Mapenzi Remix, Usia wa Babu, Mpenzi Nenda na  Wivu.
Naye Khalid Chuma Chokoraa alisema kwamba anawaalika mashabiki wa bendi hiyo waje kwa wingi leo kwani kutakuwa na burudani ya aina yake ambapo wakishuka FM Academia wakiingia Mapacha Watatu kazi itakuwa bubwa.
 Akizuungumzia safari ya muziki ya bendi hiyo Meneja Dakota amesema kwamba wamepitia misukosuko mingi, kiingilio ni sh. 10,000.Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia moja ya mazungumzo ya kikao cha utambulisho wa Birthday ya Mapacha Watatu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...