Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 29, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZIKO YA MTOTO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, PETER MANGULA MAKABURI YA KINONDONI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake, Peter Mangula, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
 Watoto wa marehemu, wakiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kumzika baba yao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, akiwaongoza sehemu ya wanafamilia kuweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wake, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
 Baadhi ya Vijana wa CCM, wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Peter Mangula, wakati wakiwasili kwenye makaburi ya Kisutu Kinondoni kwa maziko.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Peter Mangula likishushwa kaburini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko ya mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula) zilizofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko ya mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula) zilizofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim,akiwaongoza mawaziri wenzake wastaafu, kuweka mashada ya maua.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, wakiweka mashada ya maua.
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbload Slaa, akiweka Shada la maua.
Kingunge Ngambale Mwilu, akiweka shada la maua kwa niaba ya wazee.
Meya wa Ilala, Jerry Slaa,akiweka shada la maua.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...