Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 13, 2013

NDEGE 3 WAIBUKA NA SINGO MPYA
KUNDI jipya la muziki la Ndege 3, linaloundwa na wasanii watatu nyota wa muziki wa dansi nchini, limeibuka na kibao kingine kipya.

Wasanii wanaounda kundi hilo ni Khadija Mnoga (Kimobitel), Pauline Zongo na Joan Matovolwa.

Taarifa iliyotumwa na Khadija kwa blogu ya Liwazozito wiki hii, imeutaja wimbo huo kuwa ni Misukosuko.

Ndege 3wamerekodi wimbo huo kwa kushirikiana na repa machachari nchini, Grayson Semsekwa wa bendi ya Twanga Pepeta.

Khadija alisema tayari wamesharekodi audio ya wimbo huo na kuzisambaza kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini.

Amesema kwa sasa wanajiandaa kurekodi video ya wimbo huo kabla ya kuisambaza kwenye vituo vya televisheni nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...