Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 19, 2012

HABARI KATIKA PICHA

 Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twisa akizungumza na wamiliki wa vyombo vya habari (hawapo pichani) wakati wa warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI) kwa wadau mbali mbali jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwasili kwenye  Uwanja wa Kwa Mbombe katika kijiji cha Madizini, Kata ya Mtibwa mkoani  Morogoro ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Opereshi Sangara juzi. (Picha na Joseph Senga)
Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia  wanachi ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea katika mkoa wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika baadhi ya maeneo, kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika barabara ya
kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya jimbo la Ulanga  Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite. (Picha na Joseph Senga)


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...