Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 24, 2012

JESHI LA POLISI KUWACHUKULIA HATUA KALI WATAKAO HUJUMU ZOEZI LA SENSA Kamishna Paul Chagonja

Na MWANDISHI WETU

JESHI la Polisi nchini kuwachulia hatua kali kwa watu ambao  watahujumu zoezi  la sensa  ya Watu  na Makazi inayotarajiwa  kuanza Agasti 26 mwaka  huu.


Akizungumza na waandishi wa  habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja  alisema jeshi  limejipanga  katika  kuhakikisha  zoezi la sensa linafanyika  katika  hali  utulivu pasipokuwepo na uvunjifu wa amani wa kutaka kuhujumu zoezi hilo.


Chagonja alisema  kuwa watu ambao watafanya uhalifu ikiwemo kuchana karatasi za makarani wa sensa watachuliwa  hatua  kwa  kuwafikisha  mahakamani kutokana  na sheria  ya sensa.


Alisema kuwa kususia  sensa ni kosa ambapo aliwataka wenye malalamiko  kutekeleza zoezi  katika  hali  usalama  na  baadaye  baada  ya  kazi  hiyo  kukamilika  ndio wafuatilie  madai yao.


“Jeshi halitaweza kuwaacha watu ambao wanataka  kuhujumu zoezi la sensa  ambalo  liko kisheria kwa  madai  yao wanatumia  taasisi  katika  kushawishi wananchi wasijitokeze katika  zoezi ambalo  watendaji wetu  wametekeleza hadi kufikia  hapo”.alisema Chagonja.


Kwa Upande wa Mkurugenzi  wa Makosa  ya Jinai Robert Manumba alisema kuwa  tayari  jeshi la polisi  linawashikilia watu  kutokana  na  kutaka kuhujumu zoezi  hilo.


Alisema  bado wanaendelea  kufuatilia kwa karibu juu  ya  watu ambao wanashawishi wananchi kugoma  katika  kuhesabiwa  kwa  sababu zao ambazo  haziko  kisheria.
Manumba aliwataka  wananchi kushirikiana kwa  kutoa  taarifa za watu ambao wanaopita kwa kubandika  sitika katika  nyumba juu  ya  kugomea sensa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...