Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 31, 2012

LIVERPOOL MIKONONI MWA ANZHI MAKHACHKALA EUROPA LEAGUE



 MONACO, Ufaransa

Makhachkala inayopata nguvu ya kutosha kutoka kwa nyota wa zamani wa FC Barcelona, Samuel Eto'o, imejikuta akipangwa na Liverpool katika kundi  A la Europa League, pamoja na timu za Udinese na Young Boys ya Uswisi

WEKUNDU wa Anfield klabu ya Liverpool ya England, imeangukia mikononi mwa kikosi kinachonolewa Guus Hiddink kinachotumia pesa nyingi kusajili na kulipa wachezaji cha Anzhi Makhachkala ya Russia katika mechi za hatua ya makundi ya Europa League.

Makhachkala inayopata nguvu ya kutosha kutoka kwa nyota wa zamani wa FC Barcelona, Samuel Eto'o, Imejikuta akipangwa na Liverpool katika kundi  A la Europa League, pamoja na timu za Udinese na Young Boys ya Uswisi.

Newcastle United pia ya England imerejea katika soka la Ulaya na italazimika kumenyana vema kupenya hatua hii ya makundi ya awali, ambapo imepangwa pamoja na Bordeaux ya Ufaransa, Club Brugge ya Ubelgiji ma Maritimo ya Ureno katika kundi D.

Kwa upande wao Tottenham Hotspur imeangukia kundi J la Europa League, itakopimana ubavu dhidi ya Panthinaikos ya Ugiriki, Lazio ya Italia, na Maribor ya Slovenia.

Ukiondoa kundi A, D na J ya michuano hiyo, makundi mengine katika michuano ya pili kwa ukubwa ngazi ya klabu Ulaya yako kama ifauatavyo: Kundi B linatimu za Atletico Madrid, Hapoel Tel Aviv, Plzen na Academica, huku kundi C likiwa na Marseille, Fenerbahce, M’Gladbach na AEL Limassol.

Kundi E linajumuisha timu za Stuttgart, FC Copenhagen, Steuau Bucuresti na Molde, huku kundi F likiwa na PSV Eindhoven, Napoli, Dnipro na AIK Solna, wakati kundi G kuna Sporting, FC Basel, Genk na Vidoeton. Kundi H kuna Inter Milan, Rubin Kazan, FK Partizan na Neftci.

Lyon, Athletic Club, Sparta Prague na Hapoel Kiryat Shmona zimepangwa kundi F, ambapo kundi K linajumuisha Bayer Leverkusen, FC Metalist Kharkiv, Rosenborg na Rapid Vienna, huku kundi L likiwa na FC Twente, Hannover, Levante na Helsingborgs.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...