Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 31, 2012

KUTANA NA WAREMBO WENYE NDOTO ZA KUWA WANAMITINDO WA KIMATAIFA


 Mrembo Rahma Jumanne (20) (katikati) akiwa na warembo wenzake (kushoto) Badria Swale, Susan Robert (wa pili kulia) ni Everine Manfred na Cesilia Chitanda, wakipozi kwa 'Snap', wakati walipokutana kwenye Ufukwe wa Coco Beach wote wakiwa katika harakati za kupiga picha za mitindo na Movie jijini Dar es Salaam jana. 
 Rahma Jumanne, ni mzaliwa wa Mkoa wa Kigoma, amehitimu masomo ya Msingi katika Shule ya Msingi Kigoma, na kuendelea na masomo ya Sekondari katika shule ya Kinyigo na sasa anaendelea na masomo ya elimu ya juu katika Chuo cha Kampala International College (Information Technology ICT).
  Rahma Jumanne, ni mtoto wa nne katika familia yao yenye watoto wa 5, wa Mzee Jumanne.
 Rahma Jumanne, anapendeea Modelling, Muziki, Movie kusoma habari za kila siku katika magazeti na kusikiliza redio, kusoma Novel.
 Pia, Rahma Jumanne, ni mcheaji mzuri wa mpira wa Pete (Netiboli) na Basket Ball.
Rahma Jumanne,katika shughuli hizi za mitindo, anasimamiwa na Kampuni ya Next Logistics, ili aweze kufikia malengo yake na kuonyesha kipaji chake katika mitindo na mavazi. Mrembo huyu hivi sasa anafanya kazi za ICT na kampuni ya Poa Technology Ltd, akiendelea kujipanulia wigo wa ujuzi na elimu katika masuala ya ICT, katika chuo cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam. 
MDAU WA MITINDO NA UREMBO UKIHITAJI KUSHIRIKI NAYE WASILIANI NA MTANDAO HUU SIMU ZILIZOPO KATIKA UKURASA HUU.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...