Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 24, 2012

WAZIRI DKT MWAKYEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA TPA


Waziri wa Uchukuzi Dokta HARRISON MWAKYEMBE amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu EPHRAIM MGAWE-TPA pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili. Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dokta MWAKYEMBE amemteua Injinia MADENI KIPANGE kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dokta MWAKYEMBE ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo. Waziri MWAKYEMBE anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...