Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 27, 2012

MAALIM SEIF AISHANGAA DINI MPYA INAYOGOMA KUHESABIWA


MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, amesema anawasahangaa waumini wa dini mpya inayohamasisha na kuwashawishi waumini wa dini ya kiislma na watanzania kugomea zoezi la kuhesabiwa Sensa na watu na Makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana baada ya zoezi lamkusebiwa, Maalim , alisema kuwa kuna watu wachahe tu ambao hawajulikani walipoibukia ambao wanaamini kuwa wao ndiyo hasa wanaijua dini vilivyo kuliko hata wazee wao.

Aidha Maalim, aloiwataka wanavisiwani na watanzania wote kwa ujumla kuwapuuza watu hao wanaoeneza ujumbe na kampeni ya kuvuruga zoezi hili la kitaifa, na kuwataka kutoa ripoti kwa polisi haraka kwa atakayemgundua mtu wa namna hiyo, ili achukuliwa hatua za kisheria haraka.

Akifafanua zaidi, Maalim, alisema kuwa ''zoezi hili la Sensa wala si la kwanza kufanyika nchini Tanzania, na wala halikuwahi kuwa na kipingamizi na pia tangu enzi za mababu zetu na duniani kote hufanyika zoezi kama hili, wala haijawahi kutojitokeza dini ya kupinga ikidaai si halali kidini, jambo itu ambalo linashangaza sana''. alisema

UCHUNGUZI WA MAFOTO
Siku za hivi karibuni kumekuwa kukiibuka makundi kadhaa yanayojiita wanaharakani na wengine Uamsho, ambapo miongoni mwa wengi wanaounda makundi hayo ni vijana na wazee wachache ambao nao kwa namna moja ama nyingine ukifuatilia 'back ground' ya maisha yao ni wale walioishapitia misuko suko fulani ya kimaisha.

Kwa uchunguzi wa harakaharaka uliofanywa na mtandao huu, umegundua kuwa wapo vijana wengi wenye umri usiozidi miaka 40, wakiongozwa na wazee wachache kwa imani yao binafsi na wengi wao ni wale waliomrudia mungu aidha kwa kushawishiwa ama kutubia baada ya kuwa jambo fulani ambalo halimpendezi mungu kwa muda fulani.

Wengi wao utakuwa ni wake ambao aidha siku za nyuma waliwahi kuwa wavuta bangi na unga ama walevi wa kilevi chochote, ogopa sana mtu kama huyu pindi anapogundua kuwa alikuwa akipotea na kuamua kumrudia mungu basi kila kitu kwake yeye kitakuwa ni haramu kutokana na kwamba anakumbuka yale aliyokuwa akiyafanya siku za nyuma.

Kwa upande wangu sihani kama Zoezi la kuhesabiwa Waislamu kuwa linatatizo lolote kidini, na wala halihusiani na imani za kidini.

Tarehe 25/8 2012 mida ya saa 10:50 jioni mtandao huu ulipokea Meseji inayohamasisha kutoshiriki katika zoezi hilo, ambapo mwisho wa meseji hiyo ilitakiwa iandikwe katika mtandao huu ili iweze kusomwa na watu ama kuwatumia watu 10 na zaidi.

MESEJI HIYO ILIANDIKWA HIVI:- Yaa'' ALLAH'' natamka mimi ninaesoma SMS hii kwa kauli yangu na wewe ''ALLAH'' ukiwa shahidi, kwamba sito shiriki zoezi la SENSA mpaka kipengele cha ''DINI'' kiwemo katika ''DODOSO'' za ''SENSA''. Sitoshiriki maana huo ndio msimamo wa ''WAISLAMU'', na kama nitashiriki, allah unajua nini malipo ya ''WANAFIKI'' Daima narudia tena sita shiriki ''SENSA'', Ewe ALLAH  shuhudia. Tuma SMS hii kwa watu kumi kuashiria kwamba tuko pamoja tuseme hatuesabiwi SENSA.  MWISHO WA KUNUKUU MESEJI HIYO.

''Hivi mpaka unaacha kukaa na kufikilia maendeleo ya Familia yako na tanzania kwa ujumla unakaa chini na kuanza kutunga SMS kama hii ambayo haina tija kwako wala haitakungea lolote katika maisha yako unakuwa unafikilia nini, na pia unapotoa agizo kwa uliyemtumia kuwa atume kwa watu kumi, je umemtumia na vicha ya kufanya kazi hiyo?, Jamani tubadilike dunia ya sasa tunakoelekea ni maisha ya Sayansi na Teknolojia na tunaelekea Kidigital zaidi, tunatoka analogi, tusipoangalia Waislamu tutabaki na majungu tu huku wenzetu wakisonga mbele maana kila kukicha wao wanamiradi mipya na plani mpya sisi je tunanini????????? Haya ni mawazo yangu Wadau.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...