Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 21, 2012

WAZIRI MUU WA ETHIOPIA AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi wakati wa Uhaiwake akiwa kwenye majukwaa yakimataifa.Waziri Mkuu huyo uatawalawake ulikuwa na utata mwingi hasa kwa vyombo vya habari.
Meles Zenawi alipokuwa Hospitalini baada ya afyayake ilipozorota.

Mjue Zenawi na kifo chake.
TAARIFA ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa akipata matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitali, ''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki jana mwendo wa 23:40,'' taarifa hiyo imesema.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga ameiambia BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi.Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama kiongozi mashuhuri na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la afrika.Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa kuchukua mahala pake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...