Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 21, 2013

CHAMELEONE KUMGEUKIA MUNGUMSANII wa nyota wa Afrika Mashariki, Jose Chameleone ameamua kumgeukia Mungu na anatarajia kutoa kibao kipya cha gospel alichokipa jina la ‘Tubonge’.
Chameleone ambaye kwa sasa anatamba na single yake ya badilisha aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa kwa sasa anataka kumgeukia Mungu na kwa kuanza anatoa wimbo huo ambao ni shukrani kwa Mungu.
“Tunamuhitaji Mungu kwa wakati huu. Hasa katika kipindi hiki cha hukumu.” Aliandika Chameleone katika ukurasa wake kuwaeleza mashabiki wake wa muziki duniani kote.
Wimbo huo utakuwa wa pili kwa Chameleone utakuwa ni wa pili wake kwani awali aliwahi kushirikishwa na msanii wa Zambia, Mampi wimbo ulioitwa Nimakwanisa ambao umefanya vizuri sana barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...