Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 17, 2013

FLOYD MAYWEATHER SASA KUZIPIGA NA AMIR KHAN
BAADA ya kumchakaza Canelo Alvarez, bondia Floyd Mayweather ‘Cash Money’ anamtaka bondia wa England, Amir Khan katika mpambano unaofuata.
Kituo kinachoonyesha mapambano ya ngumi ya Mayweather cha Showtime Sports kimetoa taarifa kuwa kuna uwezekano wa bondia huyo kupambana na Khan ambaye anayatajia kutetea taji lake la IBF uzito wa welter na Devon Alexander mwezi Desemba mwaka huu jijini New York.
Mapambano mawili kati ya sita ya Mayweather yataonyeshwa moja kwa moja kupitia kituo hicho na Mkurugenzi wa Showtime Sports, Stephen Espinoza alisema kuwa wanapenda kuona mpambano huo unafanyika.
Mkurugenzi huyo amepoendekeza mpambano huo unaweza kufanyika Uingereza. "Amir Khan ni mpinzani mzuri wa Floyd Mayweather, kwa sababu ana kasi ulingoni," alisema Espinoza.
"Mpambano huo wa kuvutia unaweza kufanyika Uingereza au New York. Floyd amezungumzia uwezekano wa kufanyika kwa mpambano huo sehemu moja kati ya hizo mbili.
Kama Khan akikubali kupambana na Mayweather, analipwa fedha nyingi sana ambazo anaweza kuwa hajawahi kupata katika maisha yake ya ngumi.
Alvarez alipata pauni 7.9 milioni poamoja na kupoteza mpambano huo. Espinoza alisema kwamba Khan anaweza kuwaongezea soko kubwa katika mpambano huo kuliko ilivyokuwa kwa Alvarez.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...