Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 18, 2013

KINANA ASEMA CCM HAIKO TAYARI KUBURUZWA NA WAPINZANI, IKO TAYARI KUKOSOLEWA KWA HOJA


  3 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mh. Dk Titus Kamani wakishirikiana na wananchi kusogeza matofari katika eneo itakapojengwa nyumba ya mwenyekiti wa shina namba 12 Isenge kijiji cha Igaganulwa Kata ya Dutwa ambapo Katibu Mkuu huyo amfanya harambee na kukusanya michango mbalimbali kwa ajili ya kununulia vifaa vya ujenzi wa nyumba hiyo. 4Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi Mh. Andrew Chenge wa nne kutoka kulia ni Pascal Mabiti Mkuu wa mkoa wa Simiyu wa tano wakishiriki katika zoezi la kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya mwenyekiti wa shina. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo inayojengwa katika kitongoji cha Isenge kata ya Dutwa. 7Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwa amekaa pamoja na wananchi katika mkutano wa shina namba 12 Isenge kata ya Dutwa. 8Wananchama wa CCM shina la Isenge wakimsikiliza Katibu Mkuu hayupo pichani. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia akishiriki kula chakula cha kiasili cha kisukuma kinachoitwa Michembe, kutoka kushoto ni Mh. Andrew Chenge Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi, Pascala Mabiti Mkuu wa mkoa wa Simiyuna Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani wakishiriki kula chakula hicho. 10Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akila wali pamoja na wananchi katika kata hiyo 12Wakina mama wakiendelea na biashara zao katika soko la Kata ya Dutwa ambalo limejengwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mbunge wa jimbo hilo. 13Biashara zikiendelea sokoni hapo. 14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia kushoto akiongozana na Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Mh. Andrew Chenge wakati akikagua soko hilo. 15Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiulizia bei ya Dagaa kwa Zawadi Malina Mchuuzi wa Dagaa katika soko hilo. 16Daud Njalu Silanga Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyuakinunua Kabichi kutoka kwa Marietha Maiko mchuuzi wa mbogamboga katika soko hilo lililopo kata ya Dutwa Bariadi. 18Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza katika soko la Dutwa. 19Mh. Andrew Chenge Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi akizungumza na wananchi katika soko hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...