Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 21, 2013

STEVE NYERERE KUTOA HOTUBA ZA BABA WA TAIFA TBC KUELEKEA SIKU YA KIFO CHAKE

MSANII wa filamu nchini, Steve Mangendela 'Steve Nyerere' amepata shavu la kutangaza kwa kutoa hotuba mbalimbali za baba wa taifa zitakazokuwa zikirushwa hewani na  Luninga ya TBC mpaka siku ya kilele cha kifo cha hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hotuba hizo ambazo zilikuwa zikitolewa na baba wa Taifa sasa Steve Nyerere atakuwa akizitoa kwa kuiga sauti hile hile

Msanii huyo aliyejizolea umaarufu kwa kuiga sauti za viongozi mbalimbali nchini na Duniani kwa ujumla amekuwa akipendwa na wengi kutokana na kuiga sauti ya hayati Baba wa Taifa na kufanya kuchukua jina lake moja kwa moja ambapo kwa sasa popote uendapo uwezi kumwita kwa jina la Steve bali lazima useme Steve Nyerere

kwa sasa ameingiza kazi yake mpya mtaani inayojulikana kwa jina la Before Wedding ambayo ipo mtaani ikisambazwa na kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dae rs salaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...