Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 18, 2013

SIMBA YAVUNJA REKODI TAIFA, YAICHAPA MGAMBO 6-0


Shabiki wa Simba maarufu kama Bubu ambaye alihamia Yanga lakini jana alionekana akiwa katika jukwaa la Simba akiwa amevalia jezi za Simba
KLABU ya Simba jana ilivuna ushindi mnene wa mabao baada ya kuitandika bila huruma Mgambo Shooting mabao 6-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Simba sasa roho zao kwatu baada ya kuona matunda ya mshambuliaji wao wa Kirundi, Amis Tamwe baada kukwamisha wavuni mabao manne kati ya sita yaliyofungwa katika mchezo huo huku mawili yakifungwa na Haruna Chanongo.

kwa ushindi huo Simba imefanikiwa kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi 10. 
 Muuaji wa Mgambo, Amis Tambwe akishangilia moja ya mabao yake aliyofunga katika mchezo huo
 Betram Mombeki akichuana na beki wa Mgambo katika mchezo huo
 Betram Mombeki akiruka kwanja la beki wa Mgambo
 Haruna Chanongo akimpita kipa wa Mgambo na kufunga bao lake la kwanza
Chanongo akimchosha beki wa Mgambo 

Matokeo mengine katika michezo iliyochezwa leo ya ligi hiyo, ni kama ifuatavyo

Yanga 1-1 Prisons
Ashanti 1-1 Azam FC
Coastal 1-1 Rhino Rangers
Mtibwa Sugar 0-0 Mbeya City
JKT Ruvu 0-1 Ruvu Shooting

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...