Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 30, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 LIKIENDELEA USIKU HUU NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.Muigizaji wa filamu lakini pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,aitwaye kwa jina la kisanii Shilole akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa ccm kirumba usiku huu.
Anaitwa Christian Bella ambaye alikuwa akifanya vyema sana kwenye bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
Anaitwa Neylee,msanii wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema sana kwenye anga ya muziki huo,akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea 2013.
Pichani kati ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel akiwa na marafiki zake wakilifuatilia tamasha la serengeti fiesta 2013 usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba,ambapo wakazi wa jiji la Mwanza wamejitokeza kwa wingi.
Kila kona ni ileee full maraha tuu,huku wakiburudika na vunywaji mbalimbali kutoka kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la serengeti fiesta wakishirikiana na PSI kupitia bidhaa yao ya Salama kondom.
Vijana machachari kabisa kutoka kinondoni wakitambulika kwa jina la KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za Michael Jackson mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza.
Mmoja wa sanii waliofanya vyema sana katika shindano la BSS,Walter Chilambo,akiimba usiku huu kwenye jukwaa la Serengeti fiesta.
Mashabiki wa fiesta kibao usiku huu ndani ya ccm kirumba.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...