Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 27, 2013

MWANA FA ATOA VIDEO
Na Elizabeth John

ILE video ambayo ilikua inasubiliwa kwa hamu na wadau wa muziki wa kizazi kipya nchini, ‘Bila kukunja goti’ ambayo imeimbwa na wakali wa muziki huo, Ambwene Yesaya ‘AY’ na Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ tayari imesambazwa katika vituo mbalimbali vya televisheni nchini Afrika Kusini.
Video ya wimbo huo tayari imeanza kuonekana katika vituo vya Trace, Mtv Base, Channel O na Saund City.
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, Wimbo huo umeanza kuonekana katika vituo vya Afrika Kusini na baadae kusambazwa katika vituo mbalimbali katika nchi tofauti.
Wasanii hao waliondoka nchini katikati ya mwezi huu kwaajili ya kufanya video ya wimbo huo ambao wadau mbalimbali wa muziki nchini wanaisubili kwa hamu kutokana na maneno ambayo yametawala katika wimbo huo.
Mbali na kwenda kurekodi video ya kazi hiyo, wasanii hao wameamua kuungana tena na kutengeneza nyimbo zingine zaidi ya mbili ambazo pia wanatarajia kuzisambaza hivi karibuni.
Wasanii hao ni kati ya wasanii wa bongo fleva nchini wanaofanya vizuri kutokana na kazi zao kukubalika katika tasnia ya muziki huo ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...