Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 22, 2013

SIMBA YASHIKWA TAIFA, TAMBWE BALAA


Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe akiwanyamazisha mashabiki wa Yanga baada ya kuifungia timu yake bao la pili

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wamepunguza kasi baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa kuvutia uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na Simba kulazimishwa sare hiyo lakini Mshambuliaji wake, Amis Tambwe ameendeleza makali yake baada ya kluifungia timu yake mabao yote mawili na kufanya azidi kukaa kileleni mwa orodha ya wafungaji wa mabao katika ligi hiyo kwa kufikisha mabao sita baada ya kufunga mabao manne katika mchezo uliopita dhidi ya Mgambo Shooting.

Mbeya City ambayo hii ni sare yao ya tatu mfululizo, ambapo sare yao ya kwanza walianza na Yanga jijini Mbeya, wakafuatia sare na Mtibwa katikati ya wiki, waliamua kutoka usingizi na kupata mabao yake ya kusawazisha kupitia kwa Paul Nonga na Richard Peter.
 Haruna Chanongo akiwa kibaruani katika mchezo huo
Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi alikuwepo uwanjani, akiwapungia mashabiki wa timu hiyo

MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YA LIGI 

MGAMBO 1-1 RHINO 
KAGERA 3-0 ASHANTI
PRISONS 1-1 MTIBWA 

MICHEZO YA LEO YA LIGI 


JKT RUVU         vs    JKT OLJORO            CHAMANZI
AZAM                vs    YANGA                     TAIFA
COASTAL          vs    RUVU                        MKWAKWANI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...