Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 24, 2013

TID MNYAMA AISAMBAZA 'TAMU ASALI'


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohamed ‘TID’ Ameachia kibao chake kipya hivi karibuni kinachokwenda kwa jina la ‘Tamu Asali’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, TID alisema, katika kazi hiyo kashirikiana vema na wasanii kama Cassim Mganga na Mr Blue ambao anaamini wameitendea haki kazi hiyo kutokana na uzoefu wao katika muziki.
“Nina imani itapokewa vema na mashabiki kutokana na uwepo wa wakali hao ambao wanafanya vizuri katika muziki huo na wanakubalika katika jamii,” alisema TID.
Alisema ameamua kushirikiana na wasanii hao kutokana na kuwakubali na kuzikubali kazi zao katika ‘game’, tangu akiwa mgeni katika fani hiyo.
TID, aliwataka mashabiki na wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi hiyo, ambayo anaamini ataisambaza pamoja na video yake ili kuwapa raha mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...