Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 19, 2013

NBC YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA HIJJA YA ISLAMIC BANKING


 Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (Islamic Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akikabidhi mfano wa pasi ya kuingilia katika ndege ya kwenda na kurudi makka kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya kushinda safari ya kwenda hijja, Juma Abdallah Kheri katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. NBC itagharamia gharama zote zitakazomwezesha mshindi huyo pamoja na mwenza wake atakayemchagua kwenda kuhiji Makka, Saudi Arabia baadae mwezi Oktoba. Wa pili kushoto ni mke wa Juma, Sina Abdallah bwago atakayeambatana na mumewe kwenda hijja na kulia ni Meneja Uhusiano wa NBC, Eddie Mhina.
  Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (Islamic Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia) akikabidhi mfano wa pasi ya kuingilia katika ndege ya kwenda na kurudi makka kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya kushinda safari ya kwenda hijja, Hajra Abdulrahman Ally katika hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. NBC itagharamia gharama zote zitakazomwezesha mshindi huyo pamoja na mwenza wake atakayemchagua kwenda kuhiji mjini Makka, Saudi Arabia baadae mwezi Oktoba.
 Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (Islamic Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...