Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 30, 2014

NDOVU SPECIAL MALT YASHINDA TUZO YA UBORA WA KIMATAIFA 2014 KATIKA TUZO ZA MONDE SELECTION



Meneja wa Biaya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kushoto) akizungumza na waandishi w ahabari (hawapopichani)kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa. Kulia ni Meneja masoko wa Kampun iya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah.



Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (kulia). Akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani) kuhusu tuzo iliyopata hivikaribu ni ya ubora wakimataifa.
Bia ya Ndovu yazidi kupata umaarufu katika ngazi za kimataifa kwani imezawadiwa tuzo la Ubora wa Kimataifa kwa mwaka 2014 ijulikanayo kama ‘International High Quality Trophy 2014’.



 Ndovu itapokea tuzo hiyo katika hafla itakayo fanyika Jumatatu 2 Juni 2014, mjini Bordeaux, Ufaransa.


Kwa zaidi ya miaka 3 mfululizao bia ya Ndovu Special Malt imekuwaikishinda tuzo za ‘Gold’ na ‘Grand Gold’ iliyopelekea kuzawadiwa kombe la ubora wa Kimataifa 2014.




Akizungumza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema, “Ni heshima kubwa sana kwetu kutambuliwa katika ngazi za kimataifa. Tuzo hii inatupa motisha wa kuzidi kuimarisha ubora wa Ndovu Special Malt, kuongeza ubora ili kuwaburudisha wateja wetu ziadi”.




“Tunafurahi sana kuweza kuiipa bia ya Kitanzania umaarufu duniani kutokana na ubora wake. Tungependa kuishukuru Monde Selection kwa kuaanda shindano hili ambalo linatambua na kuzawadia kilicho bora. Tuzo hii sio tu kwa TBL Ndovu Special Malt, bali ni kwa Tanzania nzima” alisema Bw. Fimbo Butullah, Meneja wa Masoko Bia ya Ndovu.

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA ZAHANAT YA TABATA NBC

 Ofisa Uhusiano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ,Dorris Malulu, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo katika Zahanati ya NBC Tabata, Dar es Salaam. Kisima hicho kilizinduliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Ilala, Angelina Malembeka.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Ilala, Willy Sangu na anaye fatia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine na kulia ni Mganga Mfawidhi Zahanati ya Tabata NBC ,Catherine Akili.
 Wauguzi wa Zahanati ,ya Tabata NBC, Dar es Salaam, wakishangilia baada ya Ofisa Uhusiano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu kukabidhi  msaada wa kisima kwa zahanati hiyo.
 Malulu akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano
 Baadhi ya wakazi wa Tabata  waliofika kwa kupata huduma za tiba katika Zahanati hiyo wakishiriki katika hafla hiyo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine, akifungua pazia kuashiria kuzindua rasmi kisima katika Zahanati ya Tabata Nbc  Dar es Salaam
 Ofisa Uhusiano kampuni hiyo,Dorris Malulu, akimkabidhi ufunguo wa kisima hicho Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, Dk. Assenga Severine,  kuashiria Uzinduzi wa Kisima ambacho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
 Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, DK Assenga Severine na Ofisa Uhusiano kampuni ya Bia Tanzania Breweries (Tbl),Dorris Malulu wakionja maji ya kisima hicho baada ya Kuzindua kisima hicho
 Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, Daktari Assenga Severine akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji Ofisa Muuguzi wa zahanati yiho Flora Amos.
Ofisa Uhusiano kampuni ya Bia Tanzania Breweries (Tbl),Dorris Malulu, akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa Wauguzi wa Zahanati hiyo.

MAKAMU WA RAIA DKT. BILAL AFUNGUA KITUO CHA TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA NA SARATANI ZA MATUMBO NA INI CHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, JIJINI DAR LEO.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) Mwakilishi wa Taasisi ya Else Kronner Fresenius Stiftung, Prof. Konrad Mebmer (wa tatu kushoto) Mwenyekiti wa Mfuko wa Magonjwa ya mfumo wa Chakula Munich nchini Ujerumani, Prof. Meinhard Classen (kulia) na Balozi mdogo wa Ujerumani nchini Tanzania, Hans Koeppel, kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kufungua rasmi Jengo la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa Hafla fupi ya ufunguzi huo iliyofanyika Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Prof. Leonard Lema (wa pili kulia) kuhusu Mashine ya kuchunguza mfumo wa Hewa na Chakula, wakati Makamu alipokuwa akitembelea jengo jipya  la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujionea mashine hizo, leo Mei 30, 2014. (wa pili kushoto) ni Mtaalam wa mfumo wa chakula, Edwaldo Komba.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Rwegasha John, kuhusu Mashine ya kuchunguza mfumo wa Hewa na Chakula, inavyoweza kufanya kazi ya kugundua uvimbe ulio tumboni kwa mgonjwa, wakati Makamu alipokuwa akitembelea jengo jipya la  la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujionea mashine hizo, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa Hafla fupi ya ufunguzi huo iliyofanyika Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo.
 Maskamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washiriki waliosaidia ujenzi wa jengo jipya la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwakilishi wa Taasisi ya Else Kronner Fresenius Stiftung, Prof. Konrad Mebmer, baada ya ufunguzi huo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wahisani.

BALOZI SEIF IDDI AKUTANA NA MKURUGENZI WA HUAWEI YA CHINA


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni  ya mtandao wa Teknolojia ya kisasa ya China   { Huawei Techonogies } Nchini Tanzania Bwana Bruce Zhang hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni  ya Huawei Technologies Nchini Tanzania Bwana Bruce Zhang akimuonyesha Balozi Seif mpango kazi wa Kampuni yake katika mfumo wa teknolojia ya kisasa.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Kampuni  ya Huawei Technologies Nchini Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bwana Bruce Zhang aliyepo kati kati yao .Kulia yao ni Mwakilishi wa Huawei Technologies Ofisi ya  Zanzibar Bwana Peter Jiang.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni  ya Huawei Technologies Nchini Tanzania Bwana Bruce Zhang akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Nyuma yake aliyevaa shati nyeupe ni Mwakilishi wa Huawei Technologies Ofisi ya  Zanzibar Bwana Peter Jiang.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*******************************
Kampuni ya Kimataifa ya mawasiliano ya Teknolojia kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China ya Huawei Technology ambayo tayari imeshafungua tawi lake Mjini Dar es salaam imeonyesha nia ya kutaka kusaidia Zanzibar kimaendeleo katika mfumo wa kisasa wa  Teknolojia.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Nchini Tanzania Bwana Bruce Zhang alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sei Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Bruce alisema Kampuni ya Huawei Technologies ambayo imepanga kutumia kiasi cha Dolla Bilioni Tano { U$ 5,000,000,000 } ndani ya kipindi cha miaka mitano katika kutekeleza miradi  ya mafunzo ya Teknolojia, fursa za masomo ya nje na Afya ikilenga zaidi kwa wananchi wakipato cha kawaida.
Alisema mafunzo ya Teknolojia ya kisasa tayari yameshaanza kutolewa na Taasisi hiyo kwa kuwapatia watendaji wa makampuni yanayotoa huduma za simu sambamba  na wanafunzi maskulini ili kuwajengea uwezo wa kazi kupitia mfumo wa kisasa wa mawasiliano.
Alieleza kwamba miradi kadhaa ya kielimu imeanzishwa na taasisi hiyo kuwapatia mafunzo wanafunzi wa  vyuo na skuli mbali mbali nchini Tanzania zikiwemo fursa za nje ya nchi pamoja na kutafuta wanafunzi  wenye vipaji maalum watakaowezeshwa kujengewa uwezo zaidi wa kielimu.
“ Tumekuwa na utaratibu wa kila mwaka ndani ya Kampuni yetu kutenga bajeti maalum kwa ajili ya mafunzo kwa wafanyakazi wa taasisi za mitandao, wanafunzi, utoaji wa vifaa kama Kompyuta pamoja na misaada katika sekta ya afya “. Alifafanua Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Huawei Technologies.
Aidha Bwana Bruce Zhang alifahamisha kwamba Kampuni yake kwa kushirikiana na taasisi za Teknolojia ya mawasiliano zimekuwa zikiendesha shindano la kutafuta mabingwa wa mitandao ya Kompyuta  { ITC – Star } ili kuzalisha wataalamu zaidi katika fani hiyo muhimu hivi sasa.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi  aliueleza ujumbe huo wa Kampuni ya Huawei Technologies kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa iko katika kipindi cha mpito ikijiandaa na mfumo wa matumizi ya Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano { E Government  } katika utendaji wa Wizara zake zote.
Balozi Seif aliutaka uongozi wa Kampuni hiyo kujitayarisha na maombi ya miradi itakayoweza kuwekeza  na taasisi hiyo hapa Zanzibar ili kwenda sambamba na Serikali katika mfumo wa matumizi hayo ya teknolojia ya kisasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi wa Huawei Technologies kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila msaada ili kuona malengo la Kampuni hiyo yanafaidisha pande zote mbili.

WATUHUMIWA WA MLIPUKO WA MABOMU JIJINI ARUSHA WAPANDISHWA KIZIMBANI


Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi.
WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.

Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni 12

Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa Kaloleni jijini hapa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walianza upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Ameongeza kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu katika baa ya Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la aina ileile liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini hapa ambapo bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta madhara .

"Aidha baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali hapa nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko ya watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na makundi ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado unaendelea ili kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika matukio ya milipuko ya mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja wa Soweto yaliyotokea mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio haya ya kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu wan chi.  
Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAANZA RASMI LEO JIJINI DAR ES SALAAM, WASHINDI WATANO KUTAFUTWA


 Msimamizi wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents, Bw Tony Akwesa akitoa maelekezo kwa washiriki waliojitokeza kwaajili ya shindano la Tanzania Movie Talents kwa kanda ya Pwani unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuchukua fomu za ushiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents lililoanza rasmi leo Kwa Kanda ya Pwani.
 Washiriki waliojitokeza kuchukua fomu za Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma fomu kwa umakini kabla ya Kujaza
 Washiriki wakipewa maelekezo na Mmoja wa wafanyakazi wa Proin Promotions
 Washiriki wakisoma fomu kwa makini
Wakielekezwa Kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents.
Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo Katika Kanda ya Pwani Ambapo usaili unaendelea kufanyika leo na kesho katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam ambapo takriba washiriki zaidi ya 250 wameweza kuchukua fomu za ushiriki wa Shindano hilo
Shindano hili ni muendelezo wa shindano la kusana vipaji vya kuigiza ambalo limefanyika tayari kwa Kanda Tano za Tanzania yaani Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Kanda ya Kaskazini na sasa tunamalizia Kanda ya Pwani ambapo washindi watano watapatikana kwa Kanda ya Pwani na kila mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi Laki Tano taslimu.
Shindano hili limelenga kuibua vipaji vilivyojificha ambavyo havikuwahi kupata nafasi ya kuonekana. 
Baada ya Wasindi watano kupatikana kwa Kanda ya Pwani, washindi takribani 20 kutoka kanda zote sita za Tanzania watawekwa katika kambi moja Jijini Dar Es Salaam na watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu Wa Sanaa kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na baadae kushindanishwa na hatimaye mshindi mmoja kupatikana na Kuibuka na zawadi nono ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Vilevile Washiriki kumi watakaopatikana katika fainali hiyo watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na watatengeneza filamu ya pamoja na hatimaye Kuweza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo

KINANA AKERWA VIONGOZI KUPORA ARDHI YA WANNCHI


 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza maswali na kuhusu kero mbalimbali walizonazo wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara kwenye mkutano wa hadhara. uliofanyika jana katika kata hiyo.
 Baada ya kusikiliza maswali mengi yakihusiha kero ya wananchi kuporwa ardhi na baadhi ya viongozi kwa kushirikiana na  baadhi ya wawekezaji, Kinana alionekana kukerwa kwa kiasi kikubwa na kadhia hiyo na kuahidi  suala hilo kwenye vikao vya ngazi ya juu vya chama kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

 Kinana alisikitishwa zaidi  baada ya kuonekana kwamba viongozi na wawekezaji wamekuwa wakitumia vyombo vya sheria ikiwemo mahakama kukandamiza haki za wananchi hao kwa kuwa wengi wao hawajui taratibu za vyombo vya sheria hata kama wana haki za msingi.
Kufuatia kero hiyo na nyingine zilizoulizwa na wananchi kwenye mikutano kwa nhyakati mbalimbali, Kinana ameahidi kuwaripoti kwa Rais Jakaya Kikwete viongozi ambao wamekuwa chanzo cha unzembe na kudumaza haki za wananchi hasa wa maeneo ya vijijini wilayani humo mkoani Manyara
Katika ziara hiyo ya siku saba mkoani Manyara,  Kinana ameambatana na Katibu wa NEC,  Itikadi  na Uenezi,  Nape Nnauye,  kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
 Baadhi ya Wanahabari walioko kwenye msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana wakiwa kazini.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
 Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
 Wananchi wa kata ya Ayamango na mabango yao.
 Wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Ayamongo,Babati Vijijini mkoani Manyara
 Katibu wa NEC Itikadi,Sisa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia  Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini,Mh.Jitu Son na viongozi mbalimbali wachama wa Wilaya na Mkoa,wakikagua moja ya jengo la mradi wa ujenzi wa chuo cha Ualimu cha Sayansi Mamire,wilayani Babati vijijini mkoani Manyara.

PICHA NA MICHUZIJR-BABATI VIJIJINI- MANYARA. 

Thursday, May 29, 2014

BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER



BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI KWA MWAKA 2014 JIJINI DAR LEO.



 Makamu wa Rais Dkt Bilal, akipokea zawadi baada ya kufungua rasmo mkutano huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi. 
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa mwaka 2014, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo mchana. Mbali na ufunguzi wa mkutano huo pia Makamu, alishuhudia hafla ya kuapishwa kwa Wakandarasi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...