Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 13, 2014

JOKATE AWATAKA WAHITIMU WA VYUO VIKUU KUJIAJIRI


 Jokate Mwegelo akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
 Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyoandaa kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
Jokate Mwegelo akiwa na mshindi wa shindano la ubunifu, Jacqueline Rimoi ambaye alimzawadia sh, 300,000 kwa kutengeneza tangazo la kunadi bidhaa za kidoti kwenye ukumbi wa Nkrumah.
**********************************************
Na Mwandishi wetu
Mbunifu wa mitindo na Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 ametoa wito kwa wanafunzi wanao hitimu vyuo vikuu nchini kujihusisha na ujasiliamali na kutumia vilivyo vipaji vyao katika kupambana na soko la ajira.

Joketi alitoa wito huo juzi wakati akitoa mada ya jins ya kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu katika kongamano la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lijulikanao kwa jina la 2014 Market Forum.

Alisema kuwa pamoja na yeye kusomea mambo ya siasa na kuhitimu digrii yake chuoni hapo, mpaka sasa hajaweza kufanyia jambo lolote taaluma hiyo zaidi ya kujiajiri kupitia kampuni yake ya Kidoti Tanzania Limited ambayo inamuingizia fedha.
Alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na ugumu wa soko la ajira na kutokana na kuamua kujiajiri kwa njia mbadala (vipaji) vyake.
 “Wakati nasoma, lengo langu kubwa lilikuwa ni kuwa mwanasiasa, nilimaliza hapa hapa Chuo Kikuu na baadaye nilishauliwa nichukua ‘masters’, nilianza kusoma, hata hivyo nilihairisha masomo hayo baada ya kuamua kuanza kuwa mbunifu na mwaka 2013 nilizindua bidhaa yangu ya nywele na nguo zijulikanazo kwa jina la ‘kidoti brand’ na sasa nimeingiza sokoni kandambili aina ya kidoti,” alisema Jokate.

Alisema kuwa alifanya utafiti wa kina ili kuteka soko la bidhaa zake na mpaka sasa anazidi kubuni aina nyingine za mitindo ya nywele, nguo, kandambili na bidhaa nyingine.
“Tusitegemee ajira kutokana na kile tulichokisomea, tunatakiwa kuwa wabunifu na kutumia vipaji vyetu, ukiweka nia tafanikiwa pamoja na ugumu wa kupata mtaji na mambo mengine, kwa kufanya hivyo utaweza kumpa ajira mtu aliyesoma zaidi yako, ipo mifano mingi duniani na matajiri wengi hawana elimu ya kutosha, ila wamekuwa wabunifu na sasa wameajiri wataalam ambao ni wasomi, hata hivyo soko la ajira ni dogo na wachache ndiyo wanabahatika kupata kazi,” alisema.
Alisema kuwa kwa sasa lengo lake kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea pamoja na kupata ushindani mkubwa katika soko kutokana na wingi wa bidhaa kama zake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...