Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 21, 2014

Floyd Mayweather we acha tu!



Floyd Mayweather we acha tu! FLOYD Joy Sinclair Mayweather ni bondia anayetamba sasa, akiwa hajapigwa hata pambano moja la ngumi za kulipwa.
Siku hizi jina lake lililozoeleka ni Floyd Mayweather, Jr. japokuwa mashabiki wake wamezoea kumwita ‘Pretty Boy’ yaani kijana mtanashati.
Mmarekani huyu mwenye umri sawa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) japokuwa kidogo kinamtangulia kwani yeye alizaliwa Februari 24, 1977 ni bingwa wa madaraja matano.
Floyd, kumwita kwa urahisi zaidi jina lake, amepata ushindi mara nane katika mashirika mbalimbali ya ndondi duniani kwenye uzani wa aina tatu tofauti.

Anatikisa ulimwengu wa ndondi sasa hivi, ambapo anasema kwa vile yeye ni sawa na shoka lisiloogopa gogo, mundu usiochagua msitu, basi mpinzani wake ajaye hana haja ya kumjua.
Wiki chache zilizopita, Mayweather alishinda kwa pointi pambano dhidi ya Marcos Maidana mjini Las Vegas na kuunganisha mataji ya uzito wa Welter, akifikisha mapambano 46 ya ndondi za kulipwa bila kupoteza hata moja.

Maidana (30) kabla ya pambano la Mayweather alikuwa na rekodi nzuri, hivyo si mbaya wala mzuri sana, maana katika mapambano 38 ameshinda 35 na kukung’utwa matatu, lakini rekodi muhimu hapa alimpiga Khan 2011.
Mayweather ni mtu ambaye jarida maarufu la ‘Ring’ katika mwaka 1998 na 2007 limemwelezea kwamba ni mwanandondi bora. Kadhalika alichaguliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ngumi Marekani (BWAA) kuwa mpiganaji wa mwaka 2007, 2008, 2010, 2012 na 2013.
Huyu ndiye anashikilia mkanda wa WBC wa uzani wa Welter; mkanda wa WBA uzani wa Super Welter, ubingwa wa WBC Super Welter na mpokezi wa mkanda wa WBC Diamond Super Welter.
Kwa sasa kwenye ulingo ndiye anashikilia rekodi ya namba moja kwenye uzani wa Welter na kwa Uingereza wanasema ndiye ‘Pound-for-Pound Boxer’ duniani.
Hata hivyo hayo ni majigambo ya kawaida ya kizalendo ya Waingereza, lakini tovuti mbalimbali zimemtaja kuwa mkali sana ikiwa ni pamoja na majarida - Ring, Sports Illustrated, ESPN, BoxRec, Fox Sports na Yahoo!
Ni Floyd huyu huyu pia ambaye alishika nafasi ya kwanza kwenye orodha za jarida la Forbes na Sports Illustrated kama mmoja wa wanamichezo 50 wanaolipwa vyema zaidi 2012 na 2013 na madai zaidi ni kwamba ndiye anayelipwa vyema zaidi.
Kwa maana hiyo, hata kujidai kwake huko ulingoni si bure kwa sababu hata kifedha anajiweza sana na hata akistaafu katika umri wake huu hana cha kupoteza.
Pengine angependa kuacha simulizi ya kutopigwa kwake katika historia japokuwa linaonekana si jambo linalompa shida sana, kwani wengine wamefika mahali sasa wanamwita ‘Money Mayweather’.
Amedumu ulingoni kwa miaka 17 akiwa anajichotea ‘pesa ndefu ndefu’ tu na inasemwa mwaka juzi alivuta mkwanja wa pauni milioni 45 katika pambano moja dhidi ya Miguel Cotto.
Katika miaka yake ya masumbwi, Floyd amejikusanyia dola za Marekani zaidi ya milioni 350 Kwenye mitandao ya jamii, imeonekana kukiwa na ushindani au utupianaji maneno kati ya mashabiki wa Floyd na wa mwanasoka mahiri wa Hispania, Cristiano Ronaldo.
Kama alivyo Floyd kwenye ngumi katika uzani huo, Ronaldo sasa ndiye mwanasoka bora duniani baada ya kumvua ukuu huo Lionel Messi.
Floyd alizaliwa Grand Rapids, Michigan kwenye familia ya mabondia, ambapo baba yake, Floyd Mayweather Sr., alikuwa mwanamasumbwi katika uzito wa Welter na alipambana na watu sampuli ya akina Sugar Ray Leonard.
Ndugu za baba yake, Jeff Mayweather na Roger Mayweather pia walikuwa mabondia wa kulipwa ambapo Roger ndiye kocha wa Floyd kwa sasa.
Ni kana kwamba Floyd alichaguliwa kwa ajili ya ngumi, kwani alianza hayo tangu akiwa mdogo, na alipokua akamwambia bibiye:
“Nadhani bibi yangu ndiye alikiona kipaji changu kwanza. Wakati nakua nilimwambia; ‘bibi nadhani natakiwa sasa nitafute kazi’. Yeye alinijibu; ‘hapana, endelea kupigana tu’,” Floyd anatanabaisha.
Anaongeza kwamba alipofikisha umri wa miaka tisa alikuwa akiishi kwenye viunga vya New Jersey katika nyumba ya watu wa hali ya chini na wakati mwingine hawakuwa hata na umeme na ndani ya chumba walikuwa kama watu saba hivi.
“Watu wanaponiona ninayomiliki sasa hawawezi hata kufikiria nilikotoka na nilivyokuwa kwa shida lakini mie siwezi kusahau kamwe,” anasema Floyd.
Cio…










HIZI NI DVD ZA AINA MBALIMBALI ZINAZOTOLEWA NA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION AMBAZO ZINATARAJIWA KUWA HEWANI WIKI IJAYO NA MAPAMBANO YOTE YA NGUMI YATAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO ZAIDI FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO PIGA SIMU 0713406938

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...