Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 11, 2014

KINANA AWAKUTANISHA HAMIS KIGWANGALAH NA HUSSEIN BASHE WILAYANI NZEGA


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akisalimiana na wananchi wa katika mkutano wa hadhara wa CCM katika Kata ya Ndala, wilayani Nzega, Tabora leo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM na kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Nzega Hamis Kigwangalah (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Hussein Bashe aliyetoa mchango wa sh. 50,000 za kusaidia ujenzi wa jengo la CCM tawi la Puge, wilayani Nzega leo.
Wakazi wa Kata ya Ndala, wilayani Nzega. wakishangilia kwa kuonesha ishara ya CCM wakati wa mkutano wa hadhara katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Hussein Bashe  walipokutana wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM wilayani Nzega.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana 9kulia) akisaidiwa na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Hamis Kigwangalah kujenga jengo la Hospitali ya Wilaya ya Nzega.Kinana akisalimiana na wasanii wa ngoma ya asili  waliotumbuiza wakati wa ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM Kata ya Nkiniziwa
Kinana akizungumza baada ya kukagua maabara  katika Shule ya Sekondari ya Kampala, katika Kata ya Ndala, wilayani Nzega, Tabora. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Hussein Bashe na Mbunge wa Jimbo la Nzega.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...