Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 18, 2014

BONDIA COSMAS CHEKA AHAIDI KUTETEA TAJI LAKE VIZURI 
Cosmas Cheka 'kulia' 
 
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni juni mosi kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana socil hall  wa Morogoro

akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kawa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni bondia huoyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka ambaye alikuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo

mpambano huo utakaosimamiwa na TPBO utasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakae vaana na Sadiki Yusufu wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu 

Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic Miyeyusho,Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali .Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
 
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...