Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 24, 2014

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYANI IRAMBA ,AENDELEA NA ZIARA YAKE


 Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahaya Nawanda katika kijiji cha Kiselya,wilayani Iramba,mkoani Singida,pichani kati ni Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mwigulu Nchemba.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
 . Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mh.Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Kiselya,Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
 Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza jambo na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuwasili wilayani Iramba,na msafara mzima wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukitokea Wilayani Ikungi.Kinana yuko mkoani Singida kwa ziara ya siku nane.
 Ndugu Kinana akiwa sambamba na Wananchi wakishiriki kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya katika kijiji cha Kiselya Wilayani Iramba mkoani Singida iliyojengwa kwa nguvu za Wanchi.
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mbele ya Wananchi wa Kijiji cha Kiselya,wakati wa ushiriki wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kiselya,wilayani Iramba mkoani Singida
 Wananchi wa kijiji cha Kiselya wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao,kwenye mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya kijijini hapo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kiselya waliofika kumpokea wilayani Iramba mapema leo asubuhi tayari kwa kuendelea na ziara yake wilayani humo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...