Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 22, 2014

Airtel yazindua huduma ya kipekee ya vifurushi vya data maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja

Mabalozi wa Huduma mpya ya Airtel,Ney wa Mitego,Vannessa Mdee na Barnabas wakiwa wameshikilia mabango yenye kuonyesha namba ya kujiunga na huduma hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wake uliofanyika jana usiku kwenye kiota cha Maraha cha Club Rouge ndani ya Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel  Tanzania, Levi Nyakundi akizungumza na wadau mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Balozi wa huduma hiyo mpya ya Airtel,Barnabas akitoa burudani kwa wadau waliofika ukumbini hapo.
Ney wa Mitego 
Vannessa Mdee na madansa wake ndani ya nyumba.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel jana ilizindua huduma kabambe ya Intaneti itakayojulikana kama SWITCH ON. Huduma hiyo ni maalum kwa watumiaji wa huduma za Interneti Tanzania ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kufuruhai huduma ya kipekee ya vifurushi vya data/intaneti maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel  Tanzania Bw, Levi Nyakundi alisema “ ulimwengu wa leo matumizi ya huduma za intaneti/data au mtandao hayaepukiki, ukitaka kujua kinachoendelea duniani kwa haraka basi intaneti ndio suluhisho au jawabu linapopatikana, lakini kumekua na changamoto nyingi sana hasa pale tunapohitaji intaneti bora ya kutuwezesha kufanya fasta mawasiliano na tuwapendao au tunapotaka kuunganishwa na taarifa za mambo muhimu yanayoendelea dunia kote, inawezekana kila wakati umekua ukijiuliza ni MB au GB au kifurushi gani kitakuwezesha kufanya mambo yako kuwa poa zaidi, hili ndilo lililotusukuma Airtel kukuletea wewe mteja wetu huduma hii ya kisasa na ndio maana tunakuambia SWITCH ON”

“Ukiwa na Airtel ‘SWITCH ON’ watumiaji wa huduma za Intaneti Tanzania sasa wanakila sababu yakufurahia kujipatia huduma bora zaidi kwa gharama nafuu na kufanya chaguo la kufurushi utakacho MAALUM kwa simu yako. Hii ni huduma inayoenda na wakati, inazingatia utamaduni wetu kwa kuwa ni ya kukutoshelezea hitaji lako, na gharama ni nafuu kuliko zote huku ikikuhakikishia mteja Non-stop intaneti - yaani fulu makamuzi kwa wewe mtumiaji kutokupimiwa. Huduma hii ya pia inamuwezesha mteja kuwa na chaguo la kifurushi iwe kwa SIKU, WIKI au MWEZI”

“Airtel Tanzania tumejipanga zaidi kuhakikisha tunaendelea kuwa wabunifu na kuwapatia huduma bora ya mawasiliano ya internet. Tutaendelea kufanikisha  hili kwakuwa Airtel Yatosha, Airtel Money nusu gharama, au Bure Pack ni vielelezo vya huduma bora na nafuu tunazowapatia wateja wetu kwa sasa na kuwafaidisha wateja kila siku. Hivyo leo hii SWITCH ON nimuendelezo wa kuwahudumia watumiaji wa Internet nchini Tanzania kwa kuwapa wanachokitaka bila kikwazo yaani Fulu makamuzi” aliongeza Nyakundi 

 Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo akielezea jinsi ya kutumia huduma hiyo alisema “Ni rahisi sana mteja wetu kujiunga, unatakiwa tu kupiga *148*22# ikiwa tu una simu yako yenye uwezo wa kutumia intaneti /Data kisha utaweza kujichagulia aina ya kifurushi kinachokufaa kutokana na mahitaji yako kwa kuwa vifurushi ni maalum kwa simu au kifaa utakachotumia yaani iwe unasimu ya Feature phone, au Simu mpapaso (Smart phone au Tablet sisi Airtel tumekuwekea kifurishi cha intaneti maalum kwa kila simu”

‘Vilevile kwa wale wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha pia bado wananafasi ya kujiunga na vifurushi vya intaneti vya Yatosha na ikiwa wamemaliza Data /intaneti na wanapenda kujiunga na Data pekee basi wanaweza pia KU-SWITCH ON na kuendela na makamuzi” alimalizia kusema Prisca. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...