Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 30, 2014

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA ZAHANAT YA TABATA NBC

 Ofisa Uhusiano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ,Dorris Malulu, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo katika Zahanati ya NBC Tabata, Dar es Salaam. Kisima hicho kilizinduliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Ilala, Angelina Malembeka.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Ilala, Willy Sangu na anaye fatia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine na kulia ni Mganga Mfawidhi Zahanati ya Tabata NBC ,Catherine Akili.
 Wauguzi wa Zahanati ,ya Tabata NBC, Dar es Salaam, wakishangilia baada ya Ofisa Uhusiano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu kukabidhi  msaada wa kisima kwa zahanati hiyo.
 Malulu akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano
 Baadhi ya wakazi wa Tabata  waliofika kwa kupata huduma za tiba katika Zahanati hiyo wakishiriki katika hafla hiyo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine, akifungua pazia kuashiria kuzindua rasmi kisima katika Zahanati ya Tabata Nbc  Dar es Salaam
 Ofisa Uhusiano kampuni hiyo,Dorris Malulu, akimkabidhi ufunguo wa kisima hicho Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, Dk. Assenga Severine,  kuashiria Uzinduzi wa Kisima ambacho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
 Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, DK Assenga Severine na Ofisa Uhusiano kampuni ya Bia Tanzania Breweries (Tbl),Dorris Malulu wakionja maji ya kisima hicho baada ya Kuzindua kisima hicho
 Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, Daktari Assenga Severine akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji Ofisa Muuguzi wa zahanati yiho Flora Amos.
Ofisa Uhusiano kampuni ya Bia Tanzania Breweries (Tbl),Dorris Malulu, akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa Wauguzi wa Zahanati hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...