Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 20, 2014

KHALID CHOKORAA KUPANDA ULINGONI MAY 24 KUZIPIGA NA ABDUL MANYENZAMwanamuziki na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Khalid chokoraa anategemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 katika ukumbi wa friends corner  kuzipiga na bondia chipukizi mwenye uchu wa ushindi  muda wote awpo ulingoni Abdul manyenza. Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya  kujenga mwili na ya ngumi kwa muda mrefu na amekuwa akipigana na mabondia tofautitofauti mazoezini na kuona uwezo wao ni wa kawaida, hivyo anataka kuwaonesha kama ana kipaji kingine zaidi ya kuimbia, kwa sasa amekuwa akijifua katika gym ya bigright boxing ya mwananyamala  chini ya mwalimu wake bondia  mkongwe omar athuman ‘van dame’ kwa lengo la kumsambaratisha mpinzani wake ambae amekuwa akijitapa kumfukuza chokoraaa kwa kipondo kikali arudi kuimba. Siku hiyo ya jumamosi kutakuwa na mapambano ya ubingwa kati ya Karama nyilawila na Said Mbelwa  wakigombea ubingwa wa UBO-AFRICA ,wakisindikizwa na kina chokoraa na Abdul manyenza, Suleiman Galile akimkabili Abdala Pazi ‘kiroba’ nae  bingwa wa afrika Alan kamote wataoneshana umwamba na Adam ngange, Ramadhan kumbele atazipiga na Hassan kiwale”morobest” , idd athuman na julias kisarawe, nao wababe wa majigambo Zumba kukwe wataoneshana kazi na Kamanda wa makamanda, pia kutakuwa na pambano mengine mengi tu ya utangulizi ya mabondia wa tanga watazipiga na mabondia wa dare es salaam. Kama vile Athuman boxa wa tanga atazipiga na waite juma wa chalinze, Rajabu mahoja wa tanga atazipiga na kaisi wa darn a mengineyo yenye kuleta hamasa na burudani za mchezo wa ngumi, kwa vijana kuonesha vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...