Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 20, 2014

KINANA, NAPE WATUA MANYONI MASHARIKI WAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO


 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Nape Nnauye akihutubia huku akishangilia na umati wa watu katika mkutano wa hadhara ambao pia ulihudhuriwa na Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Stendi ya Manyoni, willayani Manyoni, Singida leo. Nape amesema kitendo cha vyama vya upinzani kuunda Ukawa umekirahisishia CCM kuvishambulia vyama hivyo kwa pamoja badala ya kimoja kimoja.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Stendi ya Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba tunaitaka, lakini isiwe ya
mazingaombwe ya kukoroga vichwa vya watu. ndugu msitoane macho, tusing'oane meno kwa ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi kugeuza chai ya rangi kuwa ya maziwa"
alisema Kinana akatika mkutano huo..
 Nyumba ya zamani ya mfugaji Jonase Mihangwa mkazi wa Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni.Mfugaji huyo ambaye ni mfano wa kuigwa ameamua kuuza sehemu ya mifugo yake na kuamua kujenga nyumba ya kisasa yenye umeme wa jua.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua nyumba hiyo ya zamani iliyokuwa inatumiwa na Mfugaji Mihangwa, kabla ya kujenga nyumba ya kisasa katika Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni. Singida.
 Kinana akiangalia mifungo ya Mfugaji Mihangwa iliyobakia baada ya kuuza mingine kwa ajili ya kujenga nyumba ya kisasa. Mihangwa  anasema aliamua kuuza ng'ombe 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa.
 Kinana akizindua nyumba hiyo . Kulia ni Mfugaji Mihangwa mmiliki wa nyumba hiyo.
 Kinana akiwa na mfugaji Mihangwa baada ya kuikagua nyumba hiyo ya kisasa.
 Kinana akisaidia kumpatia tofali fundi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka wakati wa ziara yake katika Jimbo ya Manyoni Mashariki. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Vijana Makhirikhiri wa wa Kijiji cha Heka, Manyoni wakitumbuiza kwa ngoma ya asili wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka, Manyoni.
 Kinana akilakiwa na mabango katika mkutano wa hadhara katika Kijiji  cha Heka wakati wa ziara yake wilayani Manyoni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...