Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 12, 2014

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE NZEGA


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa wilaya ya Nzega kwenye mkutano uliofanyika Nzega mjini na kuwaambia wananchi hao kuwa wasisumbuke na wapinzani kwani wapinzani hawapo kwa ajili ya maslahi ya maendeleo ya wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akifafanua masuala mbali mbali yanayohusu wachimbaji wadogo wa wilaya hiyo kwenye mkutano wa hadhara ambao uliongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma moja ya mabango aliokabidhiwa na wachimbaji madini wadogo wa Nzega wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Nzega mjini,wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bukene Ndugu Sulemani Zedi na Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangalla.
Baadhi ya Wachimbaji madini wadogo walikifuatilia kwa makini hotuba za viongozi  kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Nzega mjini.
Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangalla akihutubia wananchi wa Nzega  kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Nzega ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mbunge wa Nzega aliwaambia wananchi jimbo lake kuwa  viongozi wanapaswa kuwajibika kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono wa pongezi kwa mbunge wa jimbo la Nzega Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kutoa mashine ya kutotolea vifaranga wa kikundi cha vijana jimboni hapo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa viongozi wa kata ambapo zaidi ya baiskeli 163 kwa makatibu wa matawi yote na 36 kwa makatibu wa vijana ngazi ya kata na pikipiki tatu kwa Jumuiya ngazi ya wilaya ambazo zimetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Nzega Ndugu Hussein Bashe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye viwanja vya mikutano vya Ndala
Mbunge wa jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangalla akihutubia wakazi wa kata ya Ndala kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yupo Nzega kwa ziara ya siku mbili ambapo atashiriki shughuli za kimaendeleo na kukagua uhai wa chama.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe akiwasalimia wakazi wa Ndala wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM.
Maabara ya shule ya sekondari Kampala ikiwa imekamilika kabisa, shule hii ni moja ya shule za kata zilizpo wilayani Nzega.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...