Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 27, 2014

FUA NA OMO UPAE MPAKA DUBAI YAPATA WASHINDI WA KWANZA MWANZA.Meneja Msaidizi wa Masoko wa kampuni ya Unilever Tanzania, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za majumbani ikiwemo sabuni ya Omo Bi. Brenda Okagi (L) akimkabidhi zawadi ya mfano wa tiketi Bw. Happyness Neshinga wa mkoa wa Mwanza, mara baada ya kujishindia tiketi hiyo kupitia promosheni ya 'Fua Upae Hadi Dubai'  ambapo mteja huyo alishiriki kwa kujaza fomu zilizomo kwenye bidhaa za promosheni. Hadi sasa promosheni hiyo inayofanyika kila wiki imepata washindi 6 ambao kila mmoja atapata nafasi ya kusafiri na mwenzake yeyote atakaye mchagua, ambapo washindi wengine 6 wanatarajiwa kupatikana hadi mwishoni mwa mwezi juni 2014.
Meneja wa Kanda ya Ziwa toka kampuni ya Unilever Tanzania, watengenezaji wa bidhaa za majumbani ikiwemo sabuni ya unga ya kufulia ya OMO Bw. Oscar Ogoti akimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi laki sita, mshindi wa promosheni ya OMO 'Fua Upae Hadi Dubai' Bi. Orga Masota ambaye ni mkazi wa Nyashana mkoani Mwanza.

Meneja wa Kanda ya Ziwa toka kampuni ya Unilever Tanzania, watengenezaji wa bidhaa za majumbani ikiwemo sabuni ya unga ya kufulia ya OMO Bw. Oscar Ogoti akimkabidhi fedha taslimu shilingi laki sita, mshindi wa promosheni ya OMO 'Fua Upae Hadi Dubai' Bi. Orga Masota ambaye ni mkazi wa Nyashana mkoani Mwanza, baada ya kununua OMO na kujaza fomu za shindano na hatimaye kujishindia kitita hicho kupitia bahati nasibu iliyo chezeshwa mwishoni mwa wiki hii.

Nkabaaaaaa......Laki sita taslimu zimekabidhiwa leo hii kwa Bi. Orga Masota. 

Wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kulia ni Meneja wa Kanda ya Ziwa toka kampuni ya Unilever Tanzania, watengenezaji wa bidhaa za majumbani ikiwemo sabuni ya unga ya kufulia ya OMO Bw. Oscar Ogoti, Bi. Orga Masota ambaye ni mshindi wa fedha taslimu shilingi laki 6 akifuatiwa na Happyness Neshinga ambaye ni mshindi wa tiketi ya kwenda Dubai na Meneja Msaidizi wa Masoko wa kampuni ya Unilever Tanzania Bi. Brenda Okagi
PROMOSHENI ya 'Fua Upae Hadi Dubai' ilianza mnamo mwezi wa March 2014, na inategemewa kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni 2014.

Meneja wa Kanda ya Ziwa wa kampuni ya unilever Tanzania Oscar Ogoti ametoa wito kwa wananchi na wateja wote wa mkoa wa Mwanza kuichangamkia fursa hiyo ya kipekee na kuongeza kuwa zoezi hilo na promosheni hiyo ni la ukweli hivyo hawanabudi kuipokea kwa moyo wote kwani bado zawadi nyingi zitaendelea kutolewa kwa washindi huku kampuni hiyo ikijipanga zaidi kwa siku za baadaye kuja na promosheni nyingine tofauti tofauti zenye lengo la kurejesha shukurani kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...