Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 27, 2014

KINANA AINGIA MKENGE KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA KASKAZINI


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama kwenye shamba la mkulima Khamis Idd (kushoto) katika Kijiji cha Mkenge, Jimbo la Singida Kaskazini, wakati wa ziara yake
ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akisaidia kuvuna mtama kwenye shamba la mkulima Khamis Idd katika Kijiji cha Mkenge, jimboni humo leo.
 Kinana akiweka mtama kwenye mashine ya kupembua ambapo kwa saa moja hupata magunia 6 hadi 10 ya mtama.
 Mtoto mpenda siasa Stanslaus Titi akiwa amebebwa na babake  Tito Anthony akimwangalia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyekuwa akuhutubia wananchi baada ya kushiriki kuvuna mtama kwenye shamba la Khamis Idd katika Kijiji cha Mkenge, Singida Kaskazini.
 Kinana akiwa katika vazi asili la viongozi wa kabila la Wanyaturu, akitoka baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Msange, wakati wa ziara yake Singida Kaskazini leo.
 Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu katika Kijiji cha Msisi. Singida Vijijini.
 Kinana na Nyarandu wakisaidia uweka dirisha lipokagua ujenzi wa Kiwanda cha kukamua alizeti katika Kijiji cha Mtinko, Singida Kaskazini.
 Nyarandu akiteta jambo na Kinana wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mtinko.
 Mzee mwasisi wa TANU na CCM,Marko Mumwi  (84) akiwa na kitabu cha Siasa ni Kilimo tamko lililotolewa mkoani Iringa 1972.Mumwi ambaye ana kadi ya TANU ya mwaka 1960 na ya CCM, alikuwepo wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Mkenge leo.
 Kinana akimdondoshea tone la chanjo ya polio, mtotoErick Gabriel ( miezi miwili) apokwenda kukagua Zahanati mpya ya Mkenge katika Kata ya Mkenge leo. Aliyemshika ni mama mzazi wa motto huyo,Marina Jacob.
 Kinana akitoka kukagua nyumba za waganga zilizojengwa na Mkapa Foundation katika Zahanati ya Mkenge, Singida Kaskazini.
 Kinana akishangiliwa na wananchi wakati msafara wa ke uliposimamishwa katika Kijiji cha Ilongelo
 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Kinna akizungumza nao baada ya kuzindua ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata ya Makhojoa Jimbo la Singida Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...